Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 30:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Maana mimi ni pamoja nawe, asema BWANA, nikuokoe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokutawanya, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Maana mimi niko pamoja nawe, kukuokoa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitayaangamiza kabisa mataifa yote, ambayo nilikutawanya kati yao; lakini wewe sitakuangamiza kabisa. Nitakuadhibu kadiri unavyostahili wala sitakuacha uende bila kukuadhibu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Maana mimi niko pamoja nawe, kukuokoa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitayaangamiza kabisa mataifa yote, ambayo nilikutawanya kati yao; lakini wewe sitakuangamiza kabisa. Nitakuadhibu kadiri unavyostahili wala sitakuacha uende bila kukuadhibu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Maana mimi niko pamoja nawe, kukuokoa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitayaangamiza kabisa mataifa yote, ambayo nilikutawanya kati yao; lakini wewe sitakuangamiza kabisa. Nitakuadhibu kadiri unavyostahili wala sitakuacha uende bila kukuadhibu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Mimi niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote nilikokuwa nimewatawanya, sitawaangamiza ninyi kabisa. Nitawaadhibu, lakini kwa haki. Sitawaacha kabisa bila adhabu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Mimi niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,’ asema bwana. ‘Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote ambamo miongoni mwao nimewatawanya, sitawaangamiza ninyi kabisa. Nitawaadhibu, lakini kwa haki. Sitawaacha kabisa bila adhabu.’

Tazama sura Nakili




Yeremia 30:11
29 Marejeleo ya Msalaba  

Nenda, ukanene na Daudi, BWANA asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo.


BWANA, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.


mwenye kuwaonea huruma watu maelfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.


Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.


Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.


Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe.


Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.


Ee BWANA, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza.


Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA.


Maana BWANA asema hivi, Nchi yote itakuwa ukiwa; lakini sitaikomesha kabisa.


Pandeni juu ya kuta zake mkaharibu, lakini msiharibu kabisa; ondoeni matawi yake; kwa maana si yake BWANA.


Lakini hata katika siku zile, asema BWANA, sitawakomesha ninyi kabisa.


Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.


Ikawa, nilipotoa unabii, Pelatia, mwana wa Benaya, akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu, nikasema, Ee Bwana MUNGU, je! Utawakomesha kabisa mabaki ya Israeli?


Lakini nitasaza mabaki; maana mtakuwa na baadhi ya watu watakaoukimbia upanga kati ya mataifa, mtakapokuwa mmetawanyika katika nchi za watu.


Sitatumia ukali wa hasira yangu, sitamwangamiza Efraimu tena; kwa maana mimi ni Mungu, si mwanadamu mimi; mimi ndiye aliye Mtakatifu katikati yenu; wala sitaingia ndani ya mji.


Lakini pamoja na hayo yote, watakapokuwa katika nchi ya adui zao, mimi, sitawatupa, wala sitawachukia, niwaangamize kabisa, na kulivunja agano langu pamoja nao; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao;


Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu.


kwa kuwa BWANA, Mungu wako, ni Mungu wa rehema; hatakuacha wala kukuangamiza, wala hatalisahau agano la baba zako alilowaapia.


Bwana na awe pamoja na roho yako. Neema na iwe pamoja nanyi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo