Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 3:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Lakini kitu cha aibu kimeila kazi ya baba zetu tokea ujana wetu; makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 “ ‘Tangu ujana wetu, tendo hili la aibu limeangamiza kila kitu walichotolea jasho wazee wetu: Makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 “ ‘Tangu ujana wetu, tendo hili la aibu limeangamiza kila kitu walichotolea jasho wazee wetu: Makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 “‘Tangu ujana wetu, tendo hili la aibu limeangamiza kila kitu walichotolea jasho wazee wetu: makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Tangu ujana wetu miungu ya aibu imeyala matunda ya kazi za baba zetu: makundi yao ya kondoo na ng’ombe, wana wao wa kiume na wa kike.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Tangu ujana wetu miungu ya aibu imeyala matunda ya kazi za baba zetu: makundi yao ya kondoo na ng’ombe, wana wao na binti zao.

Tazama sura Nakili




Yeremia 3:24
12 Marejeleo ya Msalaba  

Maana hesabu ya miungu yako, Ee Yuda, ni sawasawa na hesabu ya miji yako; na kama ilivyo hesabu ya njia za Yerusalemu, ndivyo mlivyosimamisha madhabahu za kitu kile cha aibu, madhabahu za kumfukizia Baali uvumba.


Mimi nilisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutoitii sauti yangu.


Basi, sasa, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa nini mnafanya uovu huu mkubwa juu ya nafsi zenu wenyewe, kujikatilia mbali mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyonyaye, mtoke kati ya Yuda, msijiachie mtu abakiye;


Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi wake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi wake wa vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake.


na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.


Mkate wangu niliokupa, unga mzuri, na mafuta, na asali, nilivyokulisha, ukaviweka mbele yao viwe harufu ya kupendeza; na ndivyo vilivyokuwa; asema Bwana MUNGU.


Pamoja na hayo uliwatwaa wana wako na binti zako, ulionizalia, ukawatoa sadaka kwao ili waliwe. Je! Mambo yako ya kikahaba ni kitu kidogo tu,


Hapo ndipo utakapozikumbuka njia zako, na kutahayarika, hapo utakapowakaribisha dada zako, walio wakubwa wako na wadogo wako; nami nitakupa hao wawe binti zako, lakini si kwa agano lako.


upate kukumbuka, na kufadhaika, usifumbue kinywa chako tena, kwa sababu ya aibu yako; hapo nitakapokusamehe yote uliyoyatenda, asema Bwana MUNGU.


Nayo itachukuliwa Ashuru, iwe zawadi kwa mfalme Yarebu; Efraimu atapata aibu, na Israeli atalionea haya shauri lake mwenyewe.


Maana hakujua ya kuwa mimi ndiye niliyempa ngano, na divai, na mafuta, na kumwongezea fedha na dhahabu, walivyovitumia kwa ajili ya Baali.


Mimi nilimkuta Israeli kama zabibu nyikani; nami niliwaona baba zenu kama matunda ya mtini yaliyoiva kwanza, msimu wake wa kwanza; lakini walikwenda Baal-Peori, wakajiweka wakfu kwa kitu cha aibu, wakawa chukizo kama kitu kile walichokipenda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo