Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 3:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Lakini mimi nilisema, Nitawezaje kukuweka pamoja na watoto, na kukupa nchi ipendezayo, urithi ulio mwema wa mataifa? Nami nikasema, Mtaniita, Baba yangu, wala hamtageuka na kuacha kunifuata.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Mwenyezi-Mungu asema, “Israeli, mimi niliwaza, laiti ningekuweka miongoni mwa wanangu, na kukupa nchi nzuri ajabu, urithi usio na kifani kati ya mataifa yote. Nilidhani ungeniita, ‘Baba Yangu’, na kamwe usingeacha kunifuata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Mwenyezi-Mungu asema, “Israeli, mimi niliwaza, laiti ningekuweka miongoni mwa wanangu, na kukupa nchi nzuri ajabu, urithi usio na kifani kati ya mataifa yote. Nilidhani ungeniita, ‘Baba Yangu’, na kamwe usingeacha kunifuata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Mwenyezi-Mungu asema, “Israeli, mimi niliwaza, laiti ningekuweka miongoni mwa wanangu, na kukupa nchi nzuri ajabu, urithi usio na kifani kati ya mataifa yote. Nilidhani ungeniita, ‘Baba Yangu’, na kamwe usingeacha kunifuata.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 “Mimi mwenyewe nilisema, “ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana na kuwapa nchi nzuri, urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’ Nilidhani mngeniita ‘Baba,’ na msingegeuka, mkaacha kunifuata.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 “Mimi mwenyewe nilisema, “ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana na kuwapa nchi nzuri, urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’ Nilidhani mngeniita ‘Baba,’ na msingegeuka, mkaacha kunifuata.

Tazama sura Nakili




Yeremia 3:19
32 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaidharau nchi ile ya kupendeza, Wala hawakuliamini neno lake.


Mipaka yangu imeangukia mahali pema, Naam, nimepata urithi mzuri.


Yeye ataniita, Wewe ni baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.


Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.


Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Abrahamu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.


Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.


Wachungaji wengi wameliharibu shamba langu la mizabibu, wamelikanyaga fungu langu chini ya miguu yao, wamefanya fungu langu zuri kuwa jangwa la ukiwa.


Wakati ule watauita Yerusalemu kiti cha enzi cha BWANA; na mataifa yote yatakusanyika huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la BWANA; wala hawatakwenda tena kwa ukaidi wa moyo wao mbaya.


Je, tokea wakati huu hutanililia, Ee Baba yangu, wewe u kiongozi wa ujana wangu?


Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema BWANA.


Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawapitisha kwenye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.


Na mji huu utakuwa kwangu jina la furaha, na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote ya dunia, watakaosikia habari ya mema yote niwatendeayo, nao wataogopa na kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na amani nitakaoupatia mji huo.


Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba.


katika siku ile niliwainulia mkono wangu, kuwatoa katika nchi ya Misri, na kuwaingiza katika nchi niliyowapelelezea, itiririkayo maziwa na asali, ambayo ni utukufu wa nchi zote;


Maana ajaye kupigana naye atatenda kadiri apendavyo, wala hapana mtu atakayesimama mbele yake; naye atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi mwake.


Tena ataingia katika hiyo nchi ya uzuri, na nchi nyingi zitapinduliwa; lakini nchi hizi zitaokolewa na mkono wake, Edomu, na Moabu, na wakuu wa watu wa Amoni.


Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataifikia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.


Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.


Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuachilia Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja.


Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.


Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, kulingana na radhi ya mapenzi yake.


Ninyi mmekuwa wana wa BWANA, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa.


Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.


Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, nendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo