Yeremia 3:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC17 Wakati ule watauita Yerusalemu kiti cha enzi cha BWANA; na mataifa yote yatakusanyika huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la BWANA; wala hawatakwenda tena kwa ukaidi wa moyo wao mbaya. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema17 Wakati huo, mji wa Yerusalemu utaitwa ‘Kiti cha Enzi cha Mwenyezi-Mungu’, na mataifa yote yatakusanyika humo mbele yangu. Hawatafuata tena ukaidi wa matendo yao. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND17 Wakati huo, mji wa Yerusalemu utaitwa ‘Kiti cha Enzi cha Mwenyezi-Mungu’, na mataifa yote yatakusanyika humo mbele yangu. Hawatafuata tena ukaidi wa matendo yao. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza17 Wakati huo, mji wa Yerusalemu utaitwa ‘Kiti cha Enzi cha Mwenyezi-Mungu’, na mataifa yote yatakusanyika humo mbele yangu. Hawatafuata tena ukaidi wa matendo yao. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu17 Wakati huo, wataita Yerusalemu kuwa Kiti cha Enzi cha Mwenyezi Mungu, nayo mataifa yote watakusanyika Yerusalemu kuliheshimu jina la Mwenyezi Mungu. Hawatafuata tena ukaidi wa mioyo yao miovu. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu17 Wakati huo, wataita Yerusalemu kuwa Kiti cha Enzi cha bwana, nayo mataifa yote watakusanyika Yerusalemu kuliheshimu jina la bwana. Hawatafuata tena ukaidi wa mioyo yao miovu. Tazama sura |
Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi.
Akaniambia, Mwanadamu, hapa ni mahali pa kiti changu cha enzi, na mahali pa nyayo za miguu yangu, nitakapokaa kati ya wana wa Israeli milele; na nyumba ya Israeli hawatalinajisi jina langu takatifu tena, wao, wala wafalme wao, kwa mambo yao ya kikahaba, na kwa mizoga ya wafalme wao, katika mahali pao pa juu;