Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 3:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Na pamoja na hayo yote dada yake, Yuda mwenye hiana, hajanirudia mimi kwa moyo wake wote, bali kwa unafiki, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Pamoja na hayo yote, Yuda, dada mdanganyifu wa Israeli, hakunirudia kwa moyo wote, bali kwa unafiki tu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Pamoja na hayo yote, Yuda, dada mdanganyifu wa Israeli, hakunirudia kwa moyo wote, bali kwa unafiki tu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Pamoja na hayo yote, Yuda, dada mdanganyifu wa Israeli, hakunirudia kwa moyo wote, bali kwa unafiki tu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Pamoja na hayo yote, Yuda dada yake mdanganyifu hakunirudia kwa moyo wake wote, bali kwa kujifanya tu,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Pamoja na hayo yote, Yuda dada yake mdanganyifu hakunirudia kwa moyo wake wote, bali kwa kujifanya tu,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 3:10
13 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Yosia akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi zote zilizokuwa milki ya wana wa Israeli, akawafanya wote walioonekana katika Israeli kutumika, naam, wamtumikie BWANA, Mungu wao. Siku zake zote hawakuacha kumfuata BWANA, Mungu wa baba zao.


Mara tu waliposikia habari zangu, wakanitii. Wageni walinijia wakinyenyekea.


Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.


Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.


Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walichonacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;


Mwelekeeni yeye mliyemwasi sana, enyi wana wa Israeli.


Wameyarudia maovu ya baba zao, waliokataa kusikia maneno yangu; wamewafuata miungu mingine na kuwatumikia; nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, wameyavunja maagano yangu niliyoyafanya na baba zao.


Umewapanda, naam, wametia mizizi, wanakua, naam, wanazaa matunda; katika vinywa vyao u karibu, bali katika mioyo yao u mbali.


Laiti kichwa changu kingekuwa maji, na macho yangu kuwa chemchemi ya machozi, ili nipate kulia mchana na usiku kwa ajili yao waliouawa wa binti ya watu wangu!


Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.


Nami nimewapiga kwa ukame na kuvu; wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu; Lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.


Yuda ametenda kwa hiana, na chukizo limetendeka katika Israeli, na katika Yerusalemu; maana Yuda ameunajisi utakatifu wa BWANA aupendao, naye amemwoa binti ya mungu mgeni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo