Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 28:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 naam, nabii Yeremia akasema, Amina, BWANA na atende hivi; BWANA ayatimize maneno yako uliyotabiri, kuvirudisha hapa vyombo vya nyumba ya BWANA na watu wote waliofungwa, toka Babeli, hadi mahali hapa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 “Na iwe hivyo! Mwenyezi-Mungu na afanye hivyo. Mwenyezi-Mungu na ayatimize maneno uliyotabiri, avirudishe hapa vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoka Babuloni pamoja na watu wote waliohamishiwa huko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 “Na iwe hivyo! Mwenyezi-Mungu na afanye hivyo. Mwenyezi-Mungu na ayatimize maneno uliyotabiri, avirudishe hapa vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoka Babuloni pamoja na watu wote waliohamishiwa huko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 “Na iwe hivyo! Mwenyezi-Mungu na afanye hivyo. Mwenyezi-Mungu na ayatimize maneno uliyotabiri, avirudishe hapa vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoka Babuloni pamoja na watu wote waliohamishiwa huko.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Akasema, “Amen! Mwenyezi Mungu na afanye hivyo! Mwenyezi Mungu na ayatimize maneno ya unabii uliyoyatoa kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba ya Mwenyezi Mungu na watu wote walio uhamishoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Akasema, “Amen! bwana na afanye hivyo! bwana na ayatimize maneno uliyotoa unabii kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba ya bwana pamoja na wote waliohamishwa.

Tazama sura Nakili




Yeremia 28:6
22 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Benaya, mwana wa Yehoyada, akamjibu mfalme, akasema, Amina; BWANA, Mungu na bwana wangu mfalme, na aseme vivyo hivyo.


Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA.


Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, Tangu milele hata milele. Watu wote na waseme, Amina. Haleluya.


Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli, Tangu milele hata milele. Amina na Amina.


Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.


Na ahimidiwe BWANA milele. Amina na Amina.


ili nipate kukitimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi itiririkayo maziwa na asali, kama ilivyo hivi leo. Ndipo nikajibu, nikasema, Amina, Ee BWANA.


Mimi hapa sikufanya haraka kuacha kuwa mchungaji nyuma yako; wala sikuitamani siku ya maradhi ya kuua; wewe unajua; yaliyotoka midomoni mwangu yalikuwa mbele za uso wako.


Je! Mabaya yalipwe badala ya mema? Maana wameichimbia nafsi yangu shimo. Kumbuka jinsi nilivyosimama mbele zako, ili niseme mema kwa ajili yao, nikaigeuze ghadhabu yako isiwapate.


Kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya BWANA, ambavyo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliviondoa kutoka mahali hapa, akavipeleka mpaka Babeli.


Pokea vitu mikononi mwa baadhi ya watu waliohamishwa, yaani, Heldai, na Tobia, na Yedaya; na siku iyo hiyo nenda ukaingie katika nyumba ya Yosia, mwana wa Sefania, waliyoifikia kutoka Babeli;


na maji yaletayo laana yatakuingia matumboni mwako, na kukuvimbisha tumbo, na kukupoozesha paja lako; na mwanamke ataitika, Amina, Amina.


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]


Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika mahali pa mjinga ataitikaje, Amina, baada ya kushukuru kwako, akiwa hayajui usemayo?


Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.


na aliye hai; nami nilikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya.


Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.


Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo