Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 26:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Mikaya Mmorashti, alitabiri katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda; akasema na watu wote wa Yuda, ya kwamba, BWANA wa majeshi asema hivi, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu, na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 “Wakati Hezekia alipokuwa mfalme wa Yuda, Mika wa Moreshethi, aliwatangazia watu wote kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi alisema hivi: ‘Mji wa Siyoni utalimwa kama shamba mji wa Yerusalemu utakuwa magofu, nao mlima wa hekalu utakuwa msitu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 “Wakati Hezekia alipokuwa mfalme wa Yuda, Mika wa Moreshethi, aliwatangazia watu wote kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi alisema hivi: ‘Mji wa Siyoni utalimwa kama shamba mji wa Yerusalemu utakuwa magofu, nao mlima wa hekalu utakuwa msitu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 “Wakati Hezekia alipokuwa mfalme wa Yuda, Mika wa Moreshethi, aliwatangazia watu wote kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi alisema hivi: ‘Mji wa Siyoni utalimwa kama shamba mji wa Yerusalemu utakuwa magofu, nao mlima wa hekalu utakuwa msitu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 “Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “ ‘Sayuni italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto, na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu kilichofunikwa na vichaka.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 “Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote: “ ‘Sayuni italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto, na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu kilichofunikwa na vichaka.’

Tazama sura Nakili




Yeremia 26:18
13 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Hukusikia wewe ya kuwa mimi ndimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale? Sasa mimi nimelitimiza jambo hili, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, hata ikawe chungu na magofu.


Hata hivyo Hezekia akajinyenyekeza kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, yeye na wenyeji wa Yerusalemu, hata haikuwajia hasira ya BWANA siku za Hezekia.


Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajitengenezea boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto?


Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako, Wamelinajisi hekalu lako takatifu. Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.


Ee mlima wangu wa uwandani, nitatoa mali zako na hazina zako zote ziwe nyara, na mahali pako palipoinuka, kwa sababu ya dhambi, katika mipaka yako yote.


Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwamwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.


Nami nitafanya Yerusalemu kuwa magofu, Makao ya mbweha; Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, Isikaliwe na mtu awaye yote.


Hili ndilo neno la BWANA lililomjia Mika, Mmoreshathi, katika siku za Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; maono aliyoyaona kuhusu Samaria na Yerusalemu.


Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.


Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.


BWANA asema hivi, Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji mwaminifu; na mlima wa BWANA wa majeshi utaitwa, mlima mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo