Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 26:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Lakini jueni hakika kwamba, mkiniua, mtajiletea juu yenu damu isiyo na hatia itakuwa juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake; kwa maana ni kweli BWANA amenituma kwenu, kuwaambieni yote mliyoyasikia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Ila jueni kwa hakika kwamba mkiniua, mtakuwa mmejiletea laana nyinyi wenyewe kwa kumwaga damu isiyo na hatia, na kuuletea laana mji huu na wakazi wake. Maana, ni kweli kwamba Mwenyezi-Mungu alinituma niwaambieni mambo hayo muyasikie.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Ila jueni kwa hakika kwamba mkiniua, mtakuwa mmejiletea laana nyinyi wenyewe kwa kumwaga damu isiyo na hatia, na kuuletea laana mji huu na wakazi wake. Maana, ni kweli kwamba Mwenyezi-Mungu alinituma niwaambieni mambo hayo muyasikie.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Ila jueni kwa hakika kwamba mkiniua, mtakuwa mmejiletea laana nyinyi wenyewe kwa kumwaga damu isiyo na hatia, na kuuletea laana mji huu na wakazi wake. Maana, ni kweli kwamba Mwenyezi-Mungu alinituma niwaambieni mambo hayo muyasikie.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, kwa kumwaga damu isiyo na hatia, mtakuwa mmejipatia dhambi juu yenu wenyewe, juu ya mji huu, na juu ya wote wanaoishi ndani yake, kwa kuwa ni kweli Mwenyezi Mungu amenituma kwenu ili niseme maneno haya masikioni mwenu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, mtakuwa mmejipatia dhambi kwa damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe, na juu ya mji huu na wote wanaoishi ndani yake, kwa maana ni kweli bwana amenituma kwenu ili niseme maneno haya yote masikioni mwenu.”

Tazama sura Nakili




Yeremia 26:15
21 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.


Reubeni akajibu, akawaambia, Sikuwaambia, nikisema, Msimkosee kijana? Wala hamkusikia; kwa hiyo tunadaiwa damu yake.


tena kwa ajili ya damu zisizo na hatia alizozimwaga; kwani aliujaza Yerusalemu damu zisizo na hatia; wala BWANA hakukubali kusamehe.


Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA na ayaangalie haya, akayalipie kisasi.


Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.


Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;


Nimewapiga watoto wako bure; hawakukubali kurudiwa; upanga wenu wenyewe umewala manabii wako, kama simba aharibuye.


Tena katika pindo za nguo zako imeonekana damu ya roho zao maskini wasio na hatia; sikuiona penye mahali palipobomoka, lakini niliiona juu ya hawa wote.


Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri.


BWANA asema hivi, Fanyeni hukumu na haki, mkamtoe yeye aliyetekwa katika mikono ya mdhalimu; wala msiwatende mabaya mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kuwadhulumu, wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia katika mahali hapa.


Ndipo Yeremia akawaambia wakuu wote na watu wote, akisema, BWANA ndiye aliyenituma kutabiri juu ya nyumba hii, na juu ya mji huu, maneno hayo yote mliyoyasikia.


Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, kusema,


kama hamwonei mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, wala kuifuata miungu mingine kwa hasara yenu wenyewe;


Hivi hamtaitia unajisi nchi ambayo mwakaa; kwa kuwa damu huitia nchi unajisi; wala hapana sadaka itoshayo kwa ajili ya nchi, kwa ajili ya damu iliyomwagwa ndani yake, isipokuwa ni damu ya huyo aliyeimwaga.


Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabi? Akamwambia, Wewe umesema.


wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate Yesu kwa hila na kumwua.


Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona kitendo cha kuuawa kwake kuwa sawa.


isije ikamwagika damu ya asiye makosa kati ya nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi, ikawa na damu juu yako.


kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; ndiyo wanayostahili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo