Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 26:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Ndipo Yeremia akawaambia wakuu wote na watu wote, akisema, BWANA ndiye aliyenituma kutabiri juu ya nyumba hii, na juu ya mji huu, maneno hayo yote mliyoyasikia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Ndipo Yeremia akawaambia wakuu na watu wote: “Mwenyezi-Mungu alinituma niwatabirie mambo yote mliyosikia nikiyasema dhidi ya hekalu hili na mji huu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Ndipo Yeremia akawaambia wakuu na watu wote: “Mwenyezi-Mungu alinituma niwatabirie mambo yote mliyosikia nikiyasema dhidi ya hekalu hili na mji huu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Ndipo Yeremia akawaambia wakuu na watu wote: “Mwenyezi-Mungu alinituma niwatabirie mambo yote mliyosikia nikiyasema dhidi ya hekalu hili na mji huu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “Mwenyezi Mungu amenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “bwana amenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia.

Tazama sura Nakili




Yeremia 26:12
9 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini jueni hakika kwamba, mkiniua, mtajiletea juu yenu damu isiyo na hatia itakuwa juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake; kwa maana ni kweli BWANA amenituma kwenu, kuwaambieni yote mliyoyasikia.


BWANA asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya BWANA, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya BWANA; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja.


Na itakuwa, wakuambiapo, Mbona unapiga kite? Ndipo utakaposema, Kwa sababu ya habari hizo, maana linakuja; na kila moyo utayeyuka, na mikono yote itakuwa dhaifu, na kila roho itazimia, na magoti yote yatageuka kuwa kama maji; tazama, linakuja, nalo litatendeka, asema Bwana MUNGU.


Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?


Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kama ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;


Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo