Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 25:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

31 Mshindo utafika hata mwisho wa dunia; Maana BWANA ana mashindano na mataifa, Atateta na watu wote wenye mwili; Na waovu atawatoa wauawe kwa upanga; asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Vishindo hivyo vitasikika hadi mwisho wa dunia, maana Mwenyezi-Mungu ana mashtaka dhidi ya mataifa; anawahukumu wanadamu wote, na waovu atawaua kwa upanga! Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Vishindo hivyo vitasikika hadi mwisho wa dunia, maana Mwenyezi-Mungu ana mashtaka dhidi ya mataifa; anawahukumu wanadamu wote, na waovu atawaua kwa upanga! Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Vishindo hivyo vitasikika hadi mwisho wa dunia, maana Mwenyezi-Mungu ana mashtaka dhidi ya mataifa; anawahukumu wanadamu wote, na waovu atawaua kwa upanga! Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia, kwa maana Mwenyezi Mungu ataleta hukumu dhidi ya mataifa; ataleta hukumu juu ya wanadamu wote na kuwaua waovu wote kwa upanga,’ ” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia, kwa maana bwana ataleta mashtaka dhidi ya mataifa; ataleta hukumu juu ya wanadamu wote na kuwaua waovu wote,’ ” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 25:31
14 Marejeleo ya Msalaba  

Makabila ya watu wamekimbia wakisikia kelele za fujo; mataifa wametawanyika ulipojiinua nafsi yako.


Maana BWANA ana ghadhabu juu ya mataifa yote, na hasira kali juu ya jeshi lao lote; amewaangamiza kabisa, amewatoa waende kuchinjwa.


Maana ni siku ya kisasi cha BWANA, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni.


Kwa maana BWANA atatoa hukumu kwa watu wote kwa moto, na kwa upanga wake, nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.


Lakini ulisema, Sina hatia mimi; bila shaka hasira yake imegeuka na kuniacha. Tazama, nitaingia hukumuni pamoja nawe, kwa sababu unasema, Sikutenda dhambi mimi.


Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni kimbunga cha tufani; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani.


Je! Unajitafutia mambo makuu? Usiyatafute; kwa maana tazama, nitaleta mabaya juu ya wote wenye mwili, asema BWANA; lakini roho yako nitakupa iwe nyara, katika mahali pote utakapokwenda.


Kwa maana siku ile i karibu, siku ile ya BWANA i karibu, siku ya mawingu; itakuwa wakati wa maangamizi kwa mataifa.


Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa kabila nyingi walio pamoja naye.


BWANA naye ana shutuma juu ya Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.


Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.


nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili ya urithi wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.


Sikieni, enyi milima, shutuma ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana shutuma na watu wake, naye atahojiana na Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo