Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 25:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Nawe utawaambia hivi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoutuma kati yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Mwenyezi-Mungu akaniamuru: “Utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Kunyweni, mlewe na kutapika; angukeni wala msiinuke tena, kwa sababu ya mauaji ninayosababisha miongoni mwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Mwenyezi-Mungu akaniamuru: “Utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Kunyweni, mlewe na kutapika; angukeni wala msiinuke tena, kwa sababu ya mauaji ninayosababisha miongoni mwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Mwenyezi-Mungu akaniamuru: “Utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Kunyweni, mlewe na kutapika; angukeni wala msiinuke tena, kwa sababu ya mauaji ninayosababisha miongoni mwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 “Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Kunyweni, mlewe na mtapike; angukeni, wala msiinuke tena kwa sababu ya upanga nitakaotuma miongoni mwenu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 “Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kunyweni, mlewe na mtapike; angukeni, wala msiinuke tena kwa sababu ya upanga nitakaotuma miongoni mwenu.’

Tazama sura Nakili




Yeremia 25:27
20 Marejeleo ya Msalaba  

Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo;


Nikayakanyaga makabila ya watu kwa hasira yangu, Nikawalevya kwa ghadhabu yangu, Nami nikaimwaga damu yao chini.


Watekao nyara wamepanda juu ya vilele vya milima katika nyika; kwa maana upanga wa BWANA utaangamiza toka upande mmoja wa nchi hata upande wa pili wa nchi; hapana mwenye mwili atakayekuwa na amani.


Ndipo utakapowaambia, BWANA asema hivi, Tazama, nitawajaza ulevi wenyeji wote wa nchi hii, hata wafalme wanaoketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na makuhani, na manabii, na wenyeji wote wa Yerusalemu.


Msimlilie aliyekufa, wala msimwombolezee, Bali mlilieni huyo aendaye zake mbali; Kwa maana yeye hatarudi tena, Wala hataiona nchi aliyozaliwa.


nao watakunywa, na kupepesuka, na kufanya wazimu, kwa sababu ya upanga nitakaoutuma kati yao.


Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi, Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.


Tangazeni habari hii katika Misri, mkaihubiri katika Migdoli, na kuihubiri katika Nofu, na Tapanesi; semeni, Simama, ujitayarishe kwa maana upanga umekula pande zako zote.


Upanga uko juu ya Wakaldayo, asema BWANA, na juu yao wakaao Babeli, na juu ya wakuu wake, na juu ya watu wake wenye hekima.


Wakiingiwa na ukali, nitawafanyia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA.


Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.


Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu, Ukaaye katika nchi ya Usi; Hata kwako kikombe kitapita, Utalewa, na kujifanya uchi.


Na hao waapao kwa dhambi ya Samaria, na kusema, Kama aishivyo Mungu wako, Ee Dani, na, Kama iishivyo njia ya Beer-sheba, hao nao wataanguka, wasiinuke tena.


Tena utalewa, utafichwa; tena utatafuta ngome kwa sababu ya adui.


Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kulia wa BWANA kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako.


Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui.


yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo