Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 23:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

30 Basi kwa sababu hiyo mimi niko juu ya manabii hao, asema BWANA, wanaompokonya kila mtu jirani yake maneno yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nitawashambulia manabii ambao wanaibiana maneno yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nitawashambulia manabii ambao wanaibiana maneno yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nitawashambulia manabii ambao wanaibiana maneno yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 “Kwa hiyo, niko kinyume na manabii wanaoibiana maneno kana kwamba ni yangu,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 “Kwa hiyo, niko kinyume na manabii wanaoibiana maneno kana kwamba ni yangu,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 23:30
14 Marejeleo ya Msalaba  

Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani.


Tazama, mimi niko juu yako, Ewe ukaaye bondeni, na kwenye jabali la uwandani, asema BWANA ninyi mnaosema, Ni nani atakayeshuka apigane nasi? Au, Ni nani atakayeingia katika makao yetu?


Tazama, mimi niko juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema,


Basi, kwa sababu hiyo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaelekeza uso wangu juu yenu, ili niwaletee mabaya, hata kukatilia mbali Yuda yote.


Na hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu, asema BWANA, kwamba mimi nitawaadhibu ninyi mahali hapa, mpate kujua ya kuwa maneno yangu yatasimama juu yenu, kuwaletea mabaya bila shaka;


Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi nazipinga hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.


Basi tazama, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu mmenena ubatili, na kuona uongo, basi, kwa sababu hiyo, mimi ni juu yenu, asema Bwana MUNGU.


Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao.


Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, na nitamtenga na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu.


Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye.


Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.


BWANA hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya BWANA na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA atalifuta jina lake chini ya mbingu.


Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana uko juu ya watenda mabaya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo