Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 23:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Kwa ajili ya hayo njia yao itakuwa kwao kama mahali pa kuteleza gizani; watateremshwa na kuanguka hapo; kwa maana nitaleta uovu juu yao, naam, mwaka wa kujiliwa kwao, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Kwa hiyo njia zao zitakuwa vichochoro vya utelezi gizani ambamo watasukumwa na kuanguka; maana, nitawaletea maafa, ufikapo mwaka wa kuwaadhibu, Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Kwa hiyo njia zao zitakuwa vichochoro vya utelezi gizani ambamo watasukumwa na kuanguka; maana, nitawaletea maafa, ufikapo mwaka wa kuwaadhibu, Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Kwa hiyo njia zao zitakuwa vichochoro vya utelezi gizani ambamo watasukumwa na kuanguka; maana, nitawaletea maafa, ufikapo mwaka wa kuwaadhibu, Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 “Kwa hiyo mapito yao yatakuwa utelezi, watafukuziwa mbali gizani na huko wataanguka. Nitaleta maafa juu yao katika mwaka wa kuadhibiwa kwao,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 “Kwa hiyo mapito yao yatakuwa utelezi, watafukuziwa mbali gizani na huko wataanguka. Nitaleta maafa juu yao katika mwaka wa kuadhibiwa kwao,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 23:12
18 Marejeleo ya Msalaba  

Atakimbizwa kutoka mwangani hata gizani, Na kufukuzwa atoke duniani.


Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa BWANA akiwafuatia.


Hakika Wewe huwaweka penye utelezi, Huwaangusha mpaka palipoharibika.


Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika.


Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.


Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.


nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapatakuwa changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.


wala hapatakuwa na mtu atakayesalia kwao; maana nitaleta mabaya juu ya watu wa Anathothi, mwaka wa kujiliwa kwao.


Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.


Aikimbiaye hofu ataanguka shimoni; na yeye atokaye shimoni atanaswa kwa mtego; maana nitaleta juu yake, yaani, juu ya Moabu, mwaka wa kujiliwa kwake, asema BWANA.


Wachinjeni mafahali wake wote; Na wateremkie machinjoni; Ole wao! Maana siku yao imewadia, Wakati wa kujiliwa kwao.


Je! Waliona aibu, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakuona aibu kabisa, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema BWANA.


Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?


Mtu aliye mwema miongoni mwao ni kama mbigili; mtu aliye mwenye adili miongoni mwao ni mbaya kuliko boma la michongoma; hiyo siku ya walinzi wako, yaani, siku ya kujiliwa kwako, imefika; sasa kutatokea kufadhaika kwao.


Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Nendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.


Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.


Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yuko katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.


ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo