Yeremia 22:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC21 Mimi nilisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutoitii sauti yangu. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema21 Mwenyezi-Mungu aliongea nanyi mlipokuwa na fanaka, lakini nyinyi mkasema, “Hatutasikiliza.” Hii ndiyo tabia yenu tangu ujana wenu, hamjapata kuitii sauti ya Mwenyezi-Mungu. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND21 Mwenyezi-Mungu aliongea nanyi mlipokuwa na fanaka, lakini nyinyi mkasema, “Hatutasikiliza.” Hii ndiyo tabia yenu tangu ujana wenu, hamjapata kuitii sauti ya Mwenyezi-Mungu. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza21 Mwenyezi-Mungu aliongea nanyi mlipokuwa na fanaka, lakini nyinyi mkasema, “Hatutasikiliza.” Hii ndiyo tabia yenu tangu ujana wenu, hamjapata kuitii sauti ya Mwenyezi-Mungu. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu21 Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama, lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’ Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako; hujanitii mimi. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu21 Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama, lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’ Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako; hujanitii mimi. Tazama sura |
Pia niliwatuma watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiwatuma pasipo kukoma, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiifuate miungu mingine, ili kuitumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza.
Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile, ambayo niliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifukiza manukato ya kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.