Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 20:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Maana kila ninenapo napiga kelele, nalia, Dhuluma na uharibifu! Kwa kuwa neno la BWANA limefanywa shutumu kwangu, na dhihaka, mchana kutwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Kila ninaposema kitu, nalalamika, napaza sauti, “Ukatili na uharibifu!” Maana kwangu kutangaza neno la Mwenyezi-Mungu kwanifanya nishutumiwe na kudhihakiwa kutwa nzima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Kila ninaposema kitu, nalalamika, napaza sauti, “Ukatili na uharibifu!” Maana kwangu kutangaza neno la Mwenyezi-Mungu kwanifanya nishutumiwe na kudhihakiwa kutwa nzima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Kila ninaposema kitu, nalalamika, napaza sauti, “Ukatili na uharibifu!” Maana kwangu kutangaza neno la Mwenyezi-Mungu kwanifanya nishutumiwe na kudhihakiwa kutwa nzima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Kila ninenapo, ninapiga kelele nikitangaza ukatili na uharibifu. Kwa hiyo neno la Mwenyezi Mungu limeniletea matukano na mashutumu mchana kutwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kila ninenapo, ninapiga kelele nikitangaza ukatili na uharibifu. Kwa hiyo neno la bwana limeniletea matukano na mashutumu mchana kutwa.

Tazama sura Nakili




Yeremia 20:8
26 Marejeleo ya Msalaba  

Akakwea kutoka huko mpaka Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa!


lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.


Mnafanya dhihaka yenu juu ya nani? Mmepanua vinywa vyenu, na kutoa ndimi zenu? Je, ninyi si wana wa uasi, uzao wa uongo;


Ole wangu, mama yangu, kwa kuwa umenizaa mtu wa kuteta, na mtu wa kushindana na dunia yote! Mimi sikukopesha kwa riba, wala watu hawakunikopesha kwa riba; lakini kila mmoja wao hunilaani.


Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.


Lakini kama hamtaki kunisikiliza, kuitakasa siku ya sabato, kutokuchukua mzigo katika malango ya Yerusalemu siku ya sabato; basi, nitawasha moto malangoni mwake, nao utaziteketeza nyumba za enzi za Yerusalemu, wala hautazimika.


Ee BWANA, umenihadaa, nami nimehadaika; wewe una nguvu kuliko mimi, ukashinda; nimekuwa kitu cha kuchekesha, mchana kutwa; kila mtu hunidhihaki.


Manabii walionitangulia, na waliokutangulia, walitabiri habari za vita, na za mabaya na za tauni juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa.


Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.


Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwamwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.


Niseme na nani na kushuhudia, wapate kusikia? Tazama, sikio lao halikutahiriwa, wala hawawezi kusikiliza; tazama, neno la BWANA limekuwa matukano kwao; hawalifurahii.


Je! Mtaiba, na kuua, na kuzini, na kuapa kwa uongo, na kumfukizia Baali uvumba, na kuifuata miungu mingine ambayo hamkuijua;


Mbona wanionesha uovu, na kunifanya nione mabaya? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea.


Mtu mmoja katika wanasheria akajibu, akamwambia, Mwalimu, kwa kusema hayo umetushutumu sisi nasi.


akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.


Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutuma yake.


Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo