Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 20:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Ee BWANA, umenihadaa, nami nimehadaika; wewe una nguvu kuliko mimi, ukashinda; nimekuwa kitu cha kuchekesha, mchana kutwa; kila mtu hunidhihaki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenidanganya, nami kweli nikadanganyika; wewe una nguvu kuliko mimi, nawe umeshinda. Kutwa nzima nimekuwa mtu wa kuchekwa, kila mtu ananidhihaki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenidanganya, nami kweli nikadanganyika; wewe una nguvu kuliko mimi, nawe umeshinda. Kutwa nzima nimekuwa mtu wa kuchekwa, kila mtu ananidhihaki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenidanganya, nami kweli nikadanganyika; wewe una nguvu kuliko mimi, nawe umeshinda. Kutwa nzima nimekuwa mtu wa kuchekwa, kila mtu ananidhihaki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Ee Mwenyezi Mungu, umenidanganya, nami nikadanganyika; wewe una nguvu kuliko mimi, nawe umenishinda. Ninadharauliwa mchana kutwa, kila mmoja ananidhihaki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Ee bwana, umenidanganya, nami nikadanganyika; wewe una nguvu kuniliko, nawe umenishinda. Ninadharauliwa mchana kutwa, kila mmoja ananidhihaki.

Tazama sura Nakili




Yeremia 20:7
32 Marejeleo ya Msalaba  

Akakwea kutoka huko mpaka Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa!


Mimi ni mtu wa kuchekwa na jirani yake, Ni mtu niliyemwita Mungu, naye akanijibu; Huyo mwenye haki, aliye mtimilifu, amekuwa ni kicheko.


Na sasa mimi nimekuwa wimbo wao, Naam, nimekuwa simo kwao.


Wenye kiburi wamenidharau mno, Lakini sikiuki sheria zako.


Maana BWANA aliniambia hivi, kwa mkono hodari, akanifundisha nisiende katika njia ya watu hawa, akisema,


Ole wangu, mama yangu, kwa kuwa umenizaa mtu wa kuteta, na mtu wa kushindana na dunia yote! Mimi sikukopesha kwa riba, wala watu hawakunikopesha kwa riba; lakini kila mmoja wao hunilaani.


Mbona maumivu yangu ni ya daima, na jeraha langu halina dawa, linakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe utakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?


Mimi hapa sikufanya haraka kuacha kuwa mchungaji nyuma yako; wala sikuitamani siku ya maradhi ya kuua; wewe unajua; yaliyotoka midomoni mwangu yalikuwa mbele za uso wako.


Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.


BWANA amekufanya kuhani badala ya Yehoyada, kuhani, ili mpate kuwa watumishi katika nyumba ya BWANA, kwa kila mtu aliye na wazimu, na kwa kila mtu ajifanyaye kuwa nabii, umtie katika mkatale na pingu.


Mfalme Sedekia akamwambia Yeremia, Nawaogopa Wayahudi waliowakimbilia Wakaldayo, wasije wakanitia katika mikono yao, nao wakanidhihaki.


Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote; Wimbo wao mchana kutwa.


Basi roho ikaniinua, ikanichukua mahali pengine; nami nikaenda kwa uchungu, na hasira kali rohoni mwangu, na mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu kwa nguvu.


Siku za kupatilizwa zimekuja, siku za kulipa zimefika; Israeli atayajua hayo; huyo nabii ni mpumbavu, huyo mtu mwenye roho ana wazimu; kwa sababu ya wingi wa uovu wako, na kwa sababu uadui umekuwa mkubwa.


Akamwomba BWANA, akasema, Nakuomba, Ee BWANA; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nilijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya.


Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa Roho ya BWANA; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubirie Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.


Basi Mafarisayo, ambao wenyewe ni wapenda fedha, waliyasikia hayo yote, wakamdhihaki.


Basi Herode akamdhalilisha, pamoja na askari wake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato.


Na baadhi ya Waepikureo na Wastoiko, wenye ujuzi, wakakutana naye. Wengine wakasema, Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza habari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo.


Basi waliposikia habari za ufufuo wa wafu wengine walifanya dhihaka; wengine wakasema, Tutakusikiliza tena kuhusu habari hiyo.


Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo wa kutofanya kazi?


wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa minyororo, na kwa kutiwa gerezani;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo