Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 20:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Lakini, Ee BWANA wa majeshi, wewe wawajaribu wenye haki, waona fikira na mioyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, wewe humthibiti mtu mwadilifu, huona yaliyo moyoni na akilini mwa watu, unijalie kuona ukiwalipiza kisasi, maana kwako nimekiweka kisa changu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, wewe humthibiti mtu mwadilifu, huona yaliyo moyoni na akilini mwa watu, unijalie kuona ukiwalipiza kisasi, maana kwako nimekiweka kisa changu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, wewe humthibiti mtu mwadilifu, huona yaliyo moyoni na akilini mwa watu, unijalie kuona ukiwalipiza kisasi, maana kwako nimekiweka kisa changu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, wewe umjaribuye mwenye haki na kupima moyo na nia, hebu nione ukilipiza kisasi juu yao, kwa maana kwako nimeliweka shauri langu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Ee bwana Mwenye Nguvu Zote, wewe umjaribuye mwenye haki na kupima moyo na nia, hebu nione ukilipiza kisasi juu yao, kwa maana kwako nimeliweka shauri langu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 20:12
26 Marejeleo ya Msalaba  

Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA na ayaangalie haya, akayalipie kisasi.


BWANA humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu.


Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;


Umenijaribu moyo wangu, umenijia usiku, Umenichunguza usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,


Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu.


Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi; Ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.


Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kutazama kwa ushindi juu ya adui zangu.


Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.


Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na fikira Ndiye Mungu aliye mwenye haki.


Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako, Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana.


Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya BWANA, akaukunjua mbele za BWANA.


Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Niliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.


Lakini, Ee BWANA wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye fikira na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.


Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba msituni; ameinua sauti yake juu yangu; kwa sababu hiyo nimemchukia.


Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.


Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.


Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.


Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.


Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.


nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.


Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, na Mkweli, utakawia hadi lini kuhukumu na kuilipa damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?


Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo