Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 20:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Lakini BWANA yuko pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawatafaulu wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Lakini wewe Mwenyezi-Mungu u pamoja nami kwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha; kwa hiyo watesi wangu watajikwaa, na hawataweza kunishinda. Wataaibika kupindukia, maana hawatafaulu. Fedheha yao itakuwa ya daima; kamwe haitasahaulika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Lakini wewe Mwenyezi-Mungu u pamoja nami kwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha; kwa hiyo watesi wangu watajikwaa, na hawataweza kunishinda. Wataaibika kupindukia, maana hawatafaulu. Fedheha yao itakuwa ya daima; kamwe haitasahaulika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Lakini wewe Mwenyezi-Mungu u pamoja nami kwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha; kwa hiyo watesi wangu watajikwaa, na hawataweza kunishinda. Wataaibika kupindukia, maana hawatafaulu. Fedheha yao itakuwa ya daima; kamwe haitasahaulika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Lakini Mwenyezi Mungu yu pamoja nami kama mpiganaji mwenye nguvu; kwa hiyo watesi wangu watajikwaa, Hawatashinda, nao wataaibika sana; aibu yao haitasahaulika milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Lakini bwana yu pamoja nami kama shujaa mwenye nguvu; hivyo washtaki wangu watajikwaa na kamwe hawatashinda. Watashindwa, nao wataaibika kabisa; kukosa adabu kwao hakutasahauliwa.

Tazama sura Nakili




Yeremia 20:11
25 Marejeleo ya Msalaba  

Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza.


Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu.


Waaibike na wafedheheke, Wote wanaotaka kuniua. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.


Kwa kuwa BWANA Aliye Juu, mwenye kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.


Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafla wataaibika.


Kwa mambo ya kutisha utatujibu, Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu. Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia, Na la bahari iliyo mbali sana,


Njoni myaone matendo ya Mungu; Hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu;


usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.


Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema BWANA, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.


Watatahayarika, naam, watafadhaika, wote pia; wale watengenezao sanamu wataingia fadhaa pamoja.


Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.


Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe.


Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.


Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.


Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA.


Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.


Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na wapenzi wako watakwenda kufungwa; hakika wakati huo utatahayarika, na kufadhaika kwa sababu ya uovu wako wote.


nami nitaleta juu yenu aibu ya milele, na fedheha ya daima, ambayo haitasahauliwa.


wewe uwarehemuye watu elfu nyingi, uwalipaye baba za watu uovu wao vifuani mwa watoto wao baada yao; Mungu aliye mkuu, aliye hodari, BWANA wa majeshi ndilo jina lake;


Tena, wengi wa hao wanaolala katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.


Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani awezaye kutupinga?


Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa kutoka kwa kinywa cha simba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo