Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 2:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Wala hawakusema, Yuko wapi BWANA, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu aliyetutoa nchini Misri, aliyetuongoza nyikani katika nchi ya jangwa na makorongo, nchi kame na yenye giza nene, nchi isiyopitiwa na mtu yeyote, wala kukaliwa na binadamu?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu aliyetutoa nchini Misri, aliyetuongoza nyikani katika nchi ya jangwa na makorongo, nchi kame na yenye giza nene, nchi isiyopitiwa na mtu yeyote, wala kukaliwa na binadamu?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu aliyetutoa nchini Misri, aliyetuongoza nyikani katika nchi ya jangwa na makorongo, nchi kame na yenye giza nene, nchi isiyopitiwa na mtu yeyote, wala kukaliwa na binadamu?’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Hawakuuliza, ‘Yuko wapi Mwenyezi Mungu, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia nyika kame, kupitia nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Hawakuuliza, ‘Yuko wapi bwana, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia nyika kame, kupitia nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’

Tazama sura Nakili




Yeremia 2:6
26 Marejeleo ya Msalaba  

Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi BWANA, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka.


Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake; Wingu na likae juu yake; Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe.


Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu, Awapaye nyimbo wakati wa usiku;


Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.


Nilifikiri habari za siku za kale, Miaka ya zamani zilizopita.


Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.


Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.


Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu.


Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.


Nenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, BWANA asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa kuposwa kwako; Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu.


Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wanasheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.


Wamemkataa BWANA, na kusema, Si yeye; wala hayatatupata mabaya; wala hatutaona upanga wala njaa;


Na wajaposema, Kama BWANA aishivyo, hakika waapa kwa uongo.


Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu yeyote, Wala hapiti mwanadamu huko.


Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri, Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.


Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu nchi ya Misri; wala hutamjua mungu mwingine ila mimi; wala zaidi ya mimi hakuna mwokozi.


Pia niliwapandisha ninyi kutoka nchi ya Misri, nikawaongoza muda wa miaka arubaini jangwani, ili mpate kuimiliki nchi ya Mwamori.


Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia.


Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama BWANA, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea.


Alimkuta katika nchi ya ukame, Na katika jangwa tupu litishalo; Alimzunguka, akamtunza; Akamhifadhi kama mboni ya jicho;


Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arubaini katika jangwa, ili akunyenyekeze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.


Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo