Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 2:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Kama mwizi aonavyo haya akamatwapo, ndivyo waonavyo haya nyumba ya Israeli; wao, na wafalme wao, na wakuu wao, na makuhani wao, na manabii wao;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 “Kama vile mwizi aonavyo aibu akishikwa, ndivyo Waisraeli watakavyoona aibu; wao wenyewe, wafalme wao, wakuu wao, makuhani wao na manabii wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 “Kama vile mwizi aonavyo aibu akishikwa, ndivyo Waisraeli watakavyoona aibu; wao wenyewe, wafalme wao, wakuu wao, makuhani wao na manabii wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 “Kama vile mwizi aonavyo aibu akishikwa, ndivyo Waisraeli watakavyoona aibu; wao wenyewe, wafalme wao, wakuu wao, makuhani wao na manabii wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 “Kama vile mwizi anavyoaibika akikamatwa, hivyo ndivyo nyumba ya Israeli inavyoaibishwa: wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao, makuhani wao na manabii wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 “Kama vile mwizi aaibikavyo wakati amekamatwa, hivyo ndivyo nyumba ya Israeli inavyoaibishwa: wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao, makuhani wao na manabii wao.

Tazama sura Nakili




Yeremia 2:26
18 Marejeleo ya Msalaba  

Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hadi leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang'anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo.


Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.


Kwa maana watatahayarika kwa sababu ya mialoni mliyoitamani, nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua.


Tazama, wenziwe wote watatahayari; na mafundi, hao ni wanadamu; na wakusanyike pamoja, wakasimame; wataogopa na kutahayari pamoja.


Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike.


Mbona unatangatanga hivi upate kugeuza mwendo wako? Utaona haya kwa ajili ya Misri pia, kama ulivyoona haya kwa ajili ya Ashuru.


Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na wapenzi wako watakwenda kufungwa; hakika wakati huo utatahayarika, na kufadhaika kwa sababu ya uovu wako wote.


kwa sababu ya mabaya yote ya wana wa Israeli, na ya wana wa Yuda, waliyoyatenda ili kunitia hasira, wao, na wafalme wao, na wakuu wao, na makuhani wao, na manabii wao, na watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu.


Na katika siku hiyo itakuwa, asema BWANA, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa.


Alionekana kati ya wezi? Maana kila umtajapo watikisa kichwa chako.


upate kuichukua aibu yako mwenyewe, na kutahayari, kwa sababu ya mambo yote uliyoyatenda, kwa kuwa umekuwa faraja kwao.


Makuhani wake wameivunja sheria yangu, wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa sikuzote; wala hawakuwafundisha watu kupambanua vitu vichafu na vitu vilivyo safi, nao wamefumba macho yao, wasiziangalie sabato zangu, nami nimetiwa unajisi kati yao.


Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.


Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo