Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 2:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 punda wa mwitu aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo katika tamaa yake; katika wakati wake ni nani awezaye kumgeuza? Wote wamtafutao hawatajichosha nafsi zao; katika mwezi wake watamwona.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 kama pundamwitu aliyezoea jangwani. Katika tamaa yake hunusanusa upepo; nani awezaye kuizuia hamu yake? Amtakaye hana haja ya kujisumbua; wakati wake ufikapo watampata tu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 kama pundamwitu aliyezoea jangwani. Katika tamaa yake hunusanusa upepo; nani awezaye kuizuia hamu yake? Amtakaye hana haja ya kujisumbua; wakati wake ufikapo watampata tu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 kama pundamwitu aliyezoea jangwani. Katika tamaa yake hunusanusa upepo; nani awezaye kuizuia hamu yake? Amtakaye hana haja ya kujisumbua; wakati wake ufikapo watampata tu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 punda-mwitu aliyezoea jangwa, anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa: wakati wake wa kuhitaji mbegu ni nani awezaye kumzuia? Madume yoyote yanayomfuatilia hayana haja ya kujichosha; wakati wa kupandwa kwake yatampata tu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 punda-mwitu aliyezoea jangwa, anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa: katika wakati wake wa kuhitaji mbegu ni nani awezaye kumzuia? Madume yoyote yanayomfuatilia hayana haja ya kujichosha; wakati wa kupandwa kwake watampata tu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 2:24
8 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu, Ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda mwitu.


Je! Waweza kuhesabu miezi yao watakayoitimiza? Au waweza kusema majira ya kuzaa kwa kulungu?


Na punda mwitu husimama juu ya vilele vya milima, Hutwetea pumzi kama mbwamwitu; Macho yao hayaoni sawasawa, Kwa kuwa hapana majani.


waliambiao gogo la mti, Wewe u baba yangu; na kuliambia jiwe, Ndiwe uliyenizaa; kwa maana wamenipa mimi visogo, wala hawakunielekezea nyuso zao; lakini wakati wa taabu watasema, Simama ukatuokoe.


Watu huwapa makahaba wote zawadi, bali wewe unawapa wapenzi wako wote zawadi zako, na kuwapa rushwa ili waje kwako pande zote, kwa ajili ya mambo yako ya kikahaba.


Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.


Kwa maana wamekwea kwenda Ashuru, mfano wa punda wa porini aliye peke yake; Efraimu ameajiri wapenzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo