Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 2:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Na sasa una nini utakayofaidi katika njia iendayo Misri, kunywa maji ya Shihori? Au una nini utakayofaidi katika njia iendayo Ashuru, kunywa maji ya ule Mto?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Na sasa itakufaa nini kwenda Misri, kunywa maji ya mto Nili? Au itakufaa nini kwenda Ashuru, kunywa maji ya mto Eufrate?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Na sasa itakufaa nini kwenda Misri, kunywa maji ya mto Nili? Au itakufaa nini kwenda Ashuru, kunywa maji ya mto Eufrate?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Na sasa itakufaa nini kwenda Misri, kunywa maji ya mto Nili? Au itakufaa nini kwenda Ashuru, kunywa maji ya mto Eufrate?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Sasa kwa nini uende Misri kunywa maji ya Shihori? Nawe kwa nini kwenda Ashuru kunywa maji ya Mto?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Sasa kwa nini uende Misri kunywa maji ya Shihori? Nawe kwa nini kwenda Ashuru kunywa maji ya Mto Frati?

Tazama sura Nakili




Yeremia 2:18
18 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa mfalme wa Ashuru ili amsaidie.


Vitu vilivyopandwa, vya Shihori, mavuno ya Nile, yaliyokuja juu ya maji mengi, ndilo pato lake, naye alikuwa soko la mataifa.


Ole wao wateremkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA!


Katika siku hiyo Bwana atanyoa kichwa na malaika ya miguuni, kwa wembe ulioajiriwa pande za ng'ambo ya Mto, yaani, kwa mfalme wa Ashuru, nao utaziondoa ndevu pia.


Mbona unatangatanga hivi upate kugeuza mwendo wako? Utaona haya kwa ajili ya Misri pia, kama ulivyoona haya kwa ajili ya Ashuru.


Utatangatanga hadi lini, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.


Macho yetu yamechoka Kwa kuutazamia bure msaada wetu; Katika kungoja kwetu tumengojea taifa Lisiloweza kutuokoa.


Tumewapa hao Wamisri mkono; Na Waashuri nao, ili tushibe chakula.


Pia umefanya mambo ya kikahaba pamoja na Waashuri, kwa sababu ulikuwa huwezi kushibishwa; naam, umefanya mambo ya kikahaba pamoja nao, wala hujashiba bado.


Lakini alimwasi kwa kutuma wajumbe huko Misri, wampe farasi na watu wengi. Je! Atafanikiwa? Afanyaye mambo hayo ataokoka? Atalivunja agano, kisha akaokoka?


Utatendwa mambo hayo kwa sababu umezini na hao wasioamini, na kwa sababu umetiwa unajisi kwa vinyago vyao.


Efraimu alipouona ugonjwa wake, na Yuda jeraha lake, ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu; lakini yeye hawezi kuwapoza, wala hatawaponya jeraha lenu.


Naye Efraimu amekuwa kama njiwa mpumbavu, asiye na fahamu; humwita Misri, huenda Ashuru.


kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; watawala watano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo