Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 2:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Tena wana wa Nofu na Tapanesi wamevunja utosi wa kichwa chako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Isitoshe, watu wa Memfisi na Tahpanesi, wameuvunja utosi wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Isitoshe, watu wa Memfisi na Tahpanesi, wameuvunja utosi wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Isitoshe, watu wa Memfisi na Tahpanesi, wameuvunja utosi wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Pia watu wa Memfisi na Tapanesi wamekupiga fuvu la kichwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Pia watu wa Memfisi na Tahpanhesi wamevunja taji ya kichwa chako.

Tazama sura Nakili




Yeremia 2:16
17 Marejeleo ya Msalaba  

Sasa tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliopondeka, yaani, Misri, ambayo mtu akiitegemea, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.


Naye Farao Neko akamfunga huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ili asitawale huko Yerusalemu. Akaitoza nchi kodi talanta mia moja za fedha na talanta ya dhahabu.


Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu, wakuu wa Nofu wamedanganyika; na hao walio mawe ya pembeni ya kabila zake wameipotosha Misri.


katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena udhalimu na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni.


naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hadi shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.


Neno lililomjia Yeremia, kuhusu Wayahudi wote waliokaa katika nchi ya Misri, waliokaa Migdoli, na Tapanesi, na Nofu, na katika nchi ya Pathrosi, kusema,


Tangazeni habari hii katika Misri, mkaihubiri katika Migdoli, na kuihubiri katika Nofu, na Tapanesi; semeni, Simama, ujitayarishe kwa maana upanga umekula pande zako zote.


Ee binti ukaaye katika Misri, Ujiweke tayari kwenda zako hali ya kufungwa; Kwa maana Nofu utakuwa ukiwa, Utateketezwa, usikaliwe na watu.


Wamekimbia, wasio na nguvu Wanasimama chini ya kivuli cha Heshboni; Ila moto umetoka katika Heshboni, Na muali wa moto toka kati ya Sihoni Nao umekula pembe ya Moabu, Na utosi wa kichwa wa watu wapigao kelele.


Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaviharibu vinyago, nami nitavikomesha vitu vya ubatili katika Nofu, wala hapatakuwa na mkuu tena atokaye katika nchi ya Misri, nami nitatia hofu katika nchi ya Misri.


Nami nitatia moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, na No itavunjika kabisa; na Nofu itakuwa na adui wakati wa mchana.


Kwa maana, tazama, wamekwenda zao ili kukimbia uharibifu, lakini Misri itawakusanya, Nofu itawazika; vitu vyao vya fedha viwapendezavyo, magugu yatavimiliki; miiba itakuwa katika hema zao.


Na Gadi akamnena, Na abarikiwe amwongezaye Gadi; Yeye hukaa kama simba mke, Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo