Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 2:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Je! Taifa wamebadili miungu yao, ingawa siyo miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa ajili ya kitu kisichofaidia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kwamba kuna taifa lililowahi kubadilisha miungu yake ingawa miungu hiyo si miungu! Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao, wakafuata miungu isiyofaa kitu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kwamba kuna taifa lililowahi kubadilisha miungu yake ingawa miungu hiyo si miungu! Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao, wakafuata miungu isiyofaa kitu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 kwamba kuna taifa lililowahi kubadilisha miungu yake ingawa miungu hiyo si miungu! Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao, wakafuata miungu isiyofaa kitu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu batili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu zisizofaa kitu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 2:11
23 Marejeleo ya Msalaba  

kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake.


Lakini malaika wa BWANA akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni?


Je! Hamkuwafukuza makuhani wa BWANA, wana wa Haruni, na Walawi; mkajifanyia makuhani kama wafanyavyo watu wa nchi nyingine? Hata yeyote ajaye kujifanya wakfu na ndama, na kondoo dume saba, aweza kuwa kuhani wa hiyo isiyo miungu.


Wakaubadili utukufu wao Kuwa mfano wa ng'ombe mla majani.


Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu.


Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.


na kuwatupa miungu yao motoni; kwa maana hao hawakuwa miungu, bali kazi ya mikono ya wanadamu; walikuwa miti na mawe, ndiyo sababu wakawaharibu.


Je! Mwanadamu ajifanyie miungu, wasio miungu?


Basi, kwa ajili ya hayo, BWANA asema hivi, Ulizeni sasa katika mataifa, ni nani aliyesikia habari za mambo kama hayo; bikira wa Israeli ametenda tendo lichukizalo sana.


BWANA asema hivi, Baba zenu waliona dhuluma gani kwangu, hata wakafarakana nami, wakafuata ubatili, nao wakawa ubatili?


Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wanasheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.


Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba.


ili niwakamate nyumba ya Israeli kwa mioyo yao wenyewe, kwa sababu wamefarakana nami kwa vinyago vyao.


Basi, kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu ninyi mmefanya ghasia kuliko mataifa wawazungukao ninyi, wala hamkuenda katika sheria zangu, wala hamkuzishika amri zangu, wala hamkutenda kama kawaida za mataifa wawazungukao;


Kwa maana mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la BWANA, Mungu wetu, milele na milele.


wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.


Basi kuhusu kuvila vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.


Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu.


Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo.


Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu; Wamenikasirisha kwa ubatili wao; Nami nitawatia wivu kwa wasio watu, Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.


U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.


Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;


Akamwita mtoto, Ikabodi, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo