Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 2:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Maana, vukeni mpaka visiwa vya Kitimu, mkaone; tumeni watu waende Kedari, mkafikiri sana; mkaone kwamba jambo kama hili limekuwa wakati wowote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Haya, vukeni bahari hadi Kupro mkaone, au tumeni watu huko Kedari wakachunguze, kama jambo kama hili limewahi kutokea:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Haya, vukeni bahari hadi Kupro mkaone, au tumeni watu huko Kedari wakachunguze, kama jambo kama hili limewahi kutokea:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Haya, vukeni bahari hadi Kupro mkaone, au tumeni watu huko Kedari wakachunguze, kama jambo kama hili limewahi kutokea:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Vuka, nenda ng’ambo hadi pwani ya Kitimu nawe uangalie, tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini, uone kama kumeshawahi kuwa kitu kama hiki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Vuka, nenda ng’ambo mpaka pwani ya Kitimu nawe uangalie, tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini, uone kama kumekuwepo kitu kama hiki.

Tazama sura Nakili




Yeremia 2:10
21 Marejeleo ya Msalaba  

Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu,


Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu BWANA ameleta mabaya haya yote juu yao.


Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani.


Basi Daudi alipokuwa mzee kwa kuishi siku nyingi; alimtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme wa Waisraeli.


Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne.


Ole wangu mimi! Kwa kuwa ni mgeni katika Mesheki; Na kufanya makao yangu Katikati ya hema za Kedari.


Kwa sababu Bwana ameniambia hivi, Katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wote wa Kedari.


Ufunuo juu ya Tiro. Toeni sauti za uchungu, enyi merikebu za Tarshishi, kwa maana umeharibika kabisa, hata hapana nyumba, hapana mahali pa kuingia; toka nchi ya Kitimu wamefunuliwa habari.


Naye akasema, Usizidi kufurahi, ewe bikira uliyeaibishwa, binti wa Sidoni, haya, ondoka, uende hadi Kitimu; huko nako hutapata raha.


Kuhusu Kedari, na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alizipiga. BWANA asema hivi, Ondokeni, pandeni hadi Kedari, mkawateke nyara wana wa mashariki.


Ukatwaa baadhi ya mavazi yako, ukajifanyia mahali palipoinuka, palipopambwa kwa rangi mbalimbali, ukafanya mambo ya kikahaba juu yake; mambo kama hayo hayatakuja wala hayatakuwako.


Arabuni, na wakuu wote wa Kedari, ndio waliokuwa wafanya biashara wa mkono wako; kwa wana-kondoo, na kondoo dume, na mbuzi; kwa hao walifanya biashara nawe.


kwa mialoni ya Bashani wamefanya makasia yako; na sitaha zako wamezifanya kwa pembe iliyotiwa kazi ya njumu katika mti wa mihugu itokayo Kitimu.


Basi, kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu ninyi mmefanya ghasia kuliko mataifa wawazungukao ninyi, wala hamkuenda katika sheria zangu, wala hamkuzishika amri zangu, wala hamkutenda kama kawaida za mataifa wawazungukao;


Baada ya hayo atauelekeza uso wake kwenye visiwa, naye atavipiga visiwa vingi; lakini mkuu mmoja ataikomesha aibu iliyoletwa na yeye; naam, aibu yake hiyo atamrudishia mwenyewe.


Maana merikebu za Kitimu zitakuja kupigana naye; basi atavunjika moyo, naye atarudi na kulighadhibikia hilo agano takatifu; na kutenda kadiri apendavyo; naam, atarudi, na kuwasikiliza walioacha hilo agano takatifu.


Lakini merikebu zitakuja kutoka pwani kwa Kitimu, Nazo zitamtaabisha Ashuru, na Eberi zitamtaabisha, Yeye naye atapata uharibifu.


Hakika habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.


Basi ikawa, wote waliolishuhudia jambo hilo wakasema, Jambo kama hili halijatendeka wala kuonekana tangu siku hiyo wana wa Israeli walipokwea kutoka katika nchi ya Misri hadi leo; haya, lifikirini, fanyeni shauri, na mliseme.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo