Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 19:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya madari yake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Nyumba za Yerusalemu na ikulu za wafalme wa Yuda, naam, nyumba zote ambazo juu ya paa zake watu walifukiza ubani kwa sayari za mbinguni, na kumiminia miungu mingine tambiko za divai, zote zitatiwa unajisi kama Tofethi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Nyumba za Yerusalemu na ikulu za wafalme wa Yuda, naam, nyumba zote ambazo juu ya paa zake watu walifukiza ubani kwa sayari za mbinguni, na kumiminia miungu mingine tambiko za divai, zote zitatiwa unajisi kama Tofethi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Nyumba za Yerusalemu na ikulu za wafalme wa Yuda, naam, nyumba zote ambazo juu ya paa zake watu walifukiza ubani kwa sayari za mbinguni, na kumiminia miungu mingine tambiko za divai, zote zitatiwa unajisi kama Tofethi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Nyumba zilizo Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, Tofethi: yaani nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani, na kumimina dhabihu za vinywaji kwa miungu mingine.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Nyumba zilizoko Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, Tofethi: yaani nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani, na kumimina dhabihu za vinywaji kwa miungu mingine.’ ”

Tazama sura Nakili




Yeremia 19:13
19 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaziacha amri zote za BWANA, Mungu wao, wajitengenezea sanamu za kusubu, yaani, ndama wawili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali.


Naye akainajisi Tofethi, iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti yake motoni kwa Moleki.


Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba ya BWANA, mfalme akazivunja, akaziteremsha huko nje, na kuyatupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.


Akazivunjavunja nguzo, akayakatakata maashera, akapajaza mahali pake mifupa ya watu.


Wamepatia moto patakatifu pako; Wamelinajisi kao la jina lako hata chini.


Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako, Wamelinajisi hekalu lako takatifu. Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.


Ufunuo juu ya bonde la maono. Sasa una nini, wewe, Hata umepanda pia juu ya madari ya nyumba?


Hivyo ndivyo nitakavyopatenda mahali hapa, asema BWANA, nao wakaao humo, hata kufanya mji huu kuwa kama Tofethi;


na Wakaldayo, wanaopigana na mji huu, watakuja, na kuutia moto mji huu, na kuuteketeza, pamoja na nyumba zake, ambazo juu ya madari yake wamemfukizia Baali uvumba, na kuwamiminia miungu mingine vinywaji, ili kunikasirisha.


Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa.


Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.


Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.


nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi.


Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile, ambayo niliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifukiza manukato ya kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.


na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya madari ya nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa BWANA na kuapa pia kwa Milkomu;


Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;


Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arubaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?


tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo