Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 19:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 na kuwaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyowavunja watu hawa, na mji huu, kama mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, kisichoweza kutengenezwa tena na kuwa kizima; nao watazika watu katika Tofethi hata pasibaki mahali pa kuzikia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 na kuwaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nasema hivi: Ndivyo nitakavyovunjavunja watu hawa na mji huu kama vile mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, hata kisiweze kamwe kutengenezwa tena. Watu watazikwa Tofethi, kwa sababu hapatakuwa na mahali pengine pa kuzikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 na kuwaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nasema hivi: Ndivyo nitakavyovunjavunja watu hawa na mji huu kama vile mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, hata kisiweze kamwe kutengenezwa tena. Watu watazikwa Tofethi, kwa sababu hapatakuwa na mahali pengine pa kuzikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 na kuwaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nasema hivi: Ndivyo nitakavyovunjavunja watu hawa na mji huu kama vile mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, hata kisiweze kamwe kutengenezwa tena. Watu watazikwa Tofethi, kwa sababu hapatakuwa na mahali pengine pa kuzikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 uwaambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi.

Tazama sura Nakili




Yeremia 19:11
13 Marejeleo ya Msalaba  

Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.


Basi msiba utampata kwa ghafla; Ghafla atavunjika, bila njia ya kupona.


Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, kinavyovunjwavunjwa kikatili, hata hakipatikani katika vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani.


Nitawagonganisha, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; sitahurumia, wala sitaachilia, wala sitarehemu, hata nisiwaangamize.


Hivyo ndivyo nitakavyopatenda mahali hapa, asema BWANA, nao wakaao humo, hata kufanya mji huu kuwa kama Tofethi;


basi, angalieni, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali, Bonde la Machinjo.


Ombolezeni, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.


Juu ya madari yote ya nyumba za Moabu, na katika njia kuu zake, pana maombolezo, kila mahali; kwa maana nimevunja Moabu kama chombo kisichopendeza, asema BWANA.


Tena itakuwa utakapokwisha kukisoma kitabu hicho, utakifungia jiwe, na kukitupa katika mto Frati;


Wana wa Sayuni wenye thamani, Walinganao na dhahabu safi, Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo, Kazi ya mikono ya mfinyanzi!


Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.


naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo