Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 18:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 ili kufanya nchi yao kuwa kitu cha kushangaza, na cha kuzomewa daima; kila mtu apitaye karibu nayo atashangaa, na kutikisa kichwa chake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Wameifanya nchi yao kuwa kitisho, kitu cha kuzomewa daima. Kila mtu apitaye huko hushangaa na kutikisa kichwa chake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Wameifanya nchi yao kuwa kitisho, kitu cha kuzomewa daima. Kila mtu apitaye huko hushangaa na kutikisa kichwa chake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Wameifanya nchi yao kuwa kitisho, kitu cha kuzomewa daima. Kila mtu apitaye huko hushangaa na kutikisa kichwa chake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Nchi yao itakuwa kitu cha kutisha, na cha kudharauliwa daima; wote wapitao karibu nayo watashangaa na kutikisa vichwa vyao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Nchi yao itaharibiwa, itakuwa kitu cha kudharauliwa daima; wote wapitao karibu nayo watashangaa na kutikisa vichwa vyao.

Tazama sura Nakili




Yeremia 18:16
35 Marejeleo ya Msalaba  

Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atashtuka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini BWANA ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya?


Kwa hiyo hasira ya BWANA imekuwa juu ya Yuda na Yerusalemu, naye amewatoa kuwa matetemeko, wawe ushangao, na mazomeo, kama muonavyo kwa macho yenu.


Nami nimekuwa wa kudharauliwa na watu, Wanionapo hutikisa vichwa vyao.


Wote wanionao hunicheka sana, Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao;


Umetufanya kuwa mithali kwa mataifa, Sababu ya kutikisa kichwa kwa watu wa nchi.


tamko alilolitamka BWANA katika habari zake ndilo hili; Bikira, binti Sayuni, anakudharau, anakudhihaki sana; binti Yerusalemu anatikisa kichwa chake juu yako.


Ndipo nilipouliza, Ee Bwana, hata lini? Naye akanijibu, Hadi miji itakapokuwa ukiwa, haina wenyeji, na nyumba zitakapokuwa hazina watu, na nchi hii itakapokuwa ganjo kabisa;


Nami nitaufanya mji huu kuwa kitu cha kushangaza watu, na kuzomewa; kila mtu apitaye karibu nao atashangaa, na kuzomea kwa sababu ya mapigo yake.


angalieni, nitatuma watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema BWANA, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyoko pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima.


Nami nitawafuatia kwa upanga, na njaa, na tauni, nami nitawatoa watupwe huku na huko katika falme zote za dunia, wawe kitu cha kulaaniwa, na cha kushangaza, na cha kuzomewa, na cha kulaumiwa, katika mataifa yote nilikowafukuza.


Maana BWANA wa majeshi Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama hasira yangu, na ghadhabu yangu, ilivyomwagwa juu ya hao wakaao Yerusalemu, ndivyo ghadhabu yangu itakavyomwagwa juu yenu, mtakapoingia Misri; nanyi mtakuwa apizo, na ajabu, na laana, na aibu; wala hamtapaona mahali hapa tena.


Nami nitawatwaa mabaki wa Yuda, walioelekeza nyuso zao kuiingia nchi ya Misri, wakae huko, nao wataangamia wote pia; wataanguka katika nchi ya Misri; wataangamia kwa upanga, na kwa njaa; watakufa, tangu wadogo hata wakubwa, kwa upanga, na kwa njaa; nao watakuwa apizo, na ajabu, na laana, na aibu.


Alionekana kati ya wezi? Maana kila umtajapo watikisa kichwa chako.


Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima.


Na Edomu atakuwa ajabu; kila mtu apitaye atashangaa, na kuzomea, kwa sababu ya mapigo yake yote.


Kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA haitakaliwa na mtu, bali itakuwa ukiwa mtupu; kila mtu apitaye karibu na Babeli atashangaa, atazomea kwa sababu ya mapigo yake yote.


Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwamwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.


Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu yeyote, Wala hapiti mwanadamu huko.


Nami nitafanya Yerusalemu kuwa magofu, Makao ya mbweha; Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, Isikaliwe na mtu awaye yote.


Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yoyote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayo Siku ya hasira yake iwakayo.


ukawaambie watu wa nchi, Bwana MUNGU asema hivi, kuhusu habari zao wakaao Yerusalemu, na katika nchi ya Israeli; Watakula chakula chao kwa kukitunza sana, na maji yao watayanywa kwa ushangao, nchi yao iwe ukiwa, kwa kukosa vitu vyote viijazavyo, kwa sababu ya udhalimu wao wote wakaao ndani yake.


Wafanya biashara kati ya makabila ya watu wakuzomea; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena milele.


basi tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu, naam, kwa sababu wamewafanya ninyi kuwa ukiwa, na kuwameza pande zote, mpate kuwa milki kwa mabaki ya mataifa, nanyi mmesemwa kwa midomo yao waongeao, na kwa masingizio ya watu;


Nami nitanyosha mkono wangu juu yao, na kuifanya nchi kuwa maganjo, tena ukiwa mbaya kuliko jangwa upande wa Dibla, katika makao yao yote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Nami nitaitia hiyo nchi ukiwa; na adui zenu watakaokaa huko wataistaajabia.


Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu wameyakataa maagizo yangu, na roho zao zimezichukia amri zangu.


Kwa maana amri za Omri ndizo zishikwazo, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, nanyi mnakwenda katika mashauri yao; ili nikufanye kuwa ukiwa, na wenyeji waliomo humo kuwa zomeo; nanyi mtayachukua matukano waliyotukanwa watu wangu.


Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa vyao, wakisema,


Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa, wakisema, Ahaa! Wewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga katika siku tatu,


ndipo atakapofanya BWANA mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.


ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua BWANA kwa ghadhabu yake na hasira zake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo