Yeremia 18:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC11 Haya! Basi, ukawaambie watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, ukisema, BWANA asema hivi, Tazama, ninafinyanga mabaya juu yenu, na kuwaza mawazo juu yenu; rudini sasa, kila mmoja na aiache njia yake mbaya; zitengenezeni njia zenu, na matendo yenu. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema11 Sasa, basi, waambie watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi Hufinyanga jambo ovu dhidi yenu na kufanya mpango dhidi yenu. Rudini na kuacha njia zenu mbaya, mkarekebishe mienendo yenu na matendo yenu. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND11 Sasa, basi, waambie watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi Hufinyanga jambo ovu dhidi yenu na kufanya mpango dhidi yenu. Rudini na kuacha njia zenu mbaya, mkarekebishe mienendo yenu na matendo yenu. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza11 Sasa, basi, waambie watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi Hufinyanga jambo ovu dhidi yenu na kufanya mpango dhidi yenu. Rudini na kuacha njia zenu mbaya, mkarekebishe mienendo yenu na matendo yenu. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu11 “Basi kwa hiyo waambie watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalemu, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Tazama! Ninaandaa maafa juu yenu, nami ninapanga mabaya dhidi yenu. Kwa hiyo geukeni kutoka njia zenu mbaya, kila mmoja wenu. Tengenezeni njia zenu na matendo yenu.’ Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu11 “Basi kwa hiyo waambie watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu, ‘Hili ndilo asemalo bwana: Tazama! Ninaandaa maafa kwa ajili yenu, nami ninabuni mabaya dhidi yenu. Kwa hiyo geukeni kutoka njia zenu mbaya, kila mmoja wenu, tengenezeni njia zenu na matendo yenu.’ Tazama sura |
Pia niliwatuma watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiwatuma pasipo kukoma, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiifuate miungu mingine, ili kuitumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza.