Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 17:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 BWANA asema hivi, Jihadharini nafsi zenu, msichukue mzigo wowote siku ya sabato, wala msiulete ndani kwa malango ya Yerusalemu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Waambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa usalama wa maisha yenu, muwe na hadhari msije mkabeba mzigo siku ya Sabato, au kuingiza mzigo mjini kupitia malango ya Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Waambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa usalama wa maisha yenu, muwe na hadhari msije mkabeba mzigo siku ya Sabato, au kuingiza mzigo mjini kupitia malango ya Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Waambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa usalama wa maisha yenu, muwe na hadhari msije mkabeba mzigo siku ya Sabato, au kuingiza mzigo mjini kupitia malango ya Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Jihadharini msije mkabeba mzigo siku ya Sabato, wala kuingiza mzigo kupitia malango ya Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Hili ndilo asemalo bwana: Jihadharini msije mkabeba mzigo siku ya Sabato, wala kuingiza mzigo kupitia malango ya Yerusalemu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 17:21
18 Marejeleo ya Msalaba  

Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.


Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.


Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote.


Kama ukigeuza mguu wako usiivunje sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;


Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.


Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.


Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.


Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu;


Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yoyote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;


Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu chochote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu,


Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;


Jihadharini nafsi zenu, basi, ili mmpende BWANA, Mungu wenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo