Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 17:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Kama kware akusanyaye makinda asiyoyaangua, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya maisha yake itamtoka, na mwisho wake atakuwa mpumbavu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mtu apataye mali isiyo halali ni kama kware akusanyaye makinda ambayo hakuyaangua: Wakati wa kilele cha ujana wake itamchopoka, na mwishoni atakuwa mtu mpumbavu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mtu apataye mali isiyo halali ni kama kware akusanyaye makinda ambayo hakuyaangua: Wakati wa kilele cha ujana wake itamchopoka, na mwishoni atakuwa mtu mpumbavu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mtu apataye mali isiyo halali ni kama kware akusanyaye makinda ambayo hakuyaangua: wakati wa kilele cha ujana wake itamchopoka, na mwishoni atakuwa mtu mpumbavu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Kama kware aanguaye mayai asiyoyataga, ndivyo alivyo mtu apataye mali kwa njia zisizo za haki. Maisha yake yatakapofika katikati, siku zitamwacha, na mwishoni atabainika kuwa mpumbavu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kama kware aanguaye mayai asiyoyataga, ndivyo alivyo mtu apataye mali kwa njia zisizo za haki. Maisha yake yafikapo katikati, siku zitamwacha, na mwishoni atabainika kuwa mpumbavu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 17:11
39 Marejeleo ya Msalaba  

Hakikusalia kitu asichokula; Kwa hiyo kufanikiwa kwake hakutadumu.


Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao, Nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao.


Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.


Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.


Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.


Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongo Ni moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti.


Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.


Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.


Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.


Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjia.


Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.


Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu! Na vyumba vyake kwa udhalimu! Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira, Wala hampi mshahara wake;


Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri.


Kwa maana, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa miongoni mwao, kila mmoja ni mtamanifu; na, tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu.


Basi, kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao na mashamba yao nitawapa wale watakaowamiliki; maana kila mmoja wao, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa, ni mtamanifu; tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu.


Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.


Wanawake wa watu wangu mnawatupa nje ya nyumba zao nzuri; watoto wao wachanga mnawanyang'anya utukufu wangu milele.


Mikono yao ni hodari kwa kutenda maovu; afisa na hakimu wanataka rushwa, mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.


Na katika siku ile nitawaadhibu hao wote warukao juu ya kizingiti, waijazao nyumba ya bwana wao udhalimu na udanganyifu.


Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.


Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.


Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.


Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?


Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na mtego, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, zinazowaingiza watu katika upotevu na uharibifu.


Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.


wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;


Na kwa tamaa yao watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; wao ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala maangamizi yao hayasinzii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo