Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 15:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejesha, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Mwenyezi-Mungu akajibu: “Kama ukinirudia nitakurudishia hali ya kwanza, nawe utanitumikia tena. Kama ukisema maneno ya maana na sio ya upuuzi, basi utakuwa msemaji wangu. Watu watakuja kujumuika nawe, wala sio wewe utakayekwenda kwao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Mwenyezi-Mungu akajibu: “Kama ukinirudia nitakurudishia hali ya kwanza, nawe utanitumikia tena. Kama ukisema maneno ya maana na sio ya upuuzi, basi utakuwa msemaji wangu. Watu watakuja kujumuika nawe, wala sio wewe utakayekwenda kwao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Mwenyezi-Mungu akajibu: “Kama ukinirudia nitakurudishia hali ya kwanza, nawe utanitumikia tena. Kama ukisema maneno ya maana na sio ya upuuzi, basi utakuwa msemaji wangu. Watu watakuja kujumuika nawe, wala sio wewe utakayekwenda kwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Ukitubu, nitakurejesha ili uweze kunitumikia; ukinena maneno yenye maana, wala si ya upuzi, utakuwa mnenaji wangu. Watu hawa ndio watakaokugeukia, wala si wewe utakayewageukia wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Kwa hiyo hili ndilo asemalo bwana: “Kama ukitubu, nitakurejeza ili uweze kunitumikia; kama ukinena maneno yenye maana, wala si ya upuzi, utakuwa mnenaji wangu. Watu hawa ndio watakaokugeukia, wala si wewe utakayewageukia wao.

Tazama sura Nakili




Yeremia 15:19
34 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.


Basi sasa, nenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena.


Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.


Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;


Ndipo BWANA akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.


Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.


basi, kwa sababu hiyo, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Yonadabu, mwana wa Rekabu, hatakosa kuwa na mzawa wa kusimama mbele zangu hata milele.


Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa;


Mifuo inafukuta kwa nguvu; risasi tu inatoka katika moto huo; mfua fedha ameyeyusha bure tu; maana wabaya hawaondolewi mbali.


Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamanio yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.


Nawe utawaambia maneno yangu, iwe watasikia au hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.


Makuhani wake wameivunja sheria yangu, wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa sikuzote; wala hawakuwafundisha watu kupambanua vitu vichafu na vitu vilivyo safi, nao wamefumba macho yao, wasiziangalie sabato zangu, nami nimetiwa unajisi kati yao.


Nao watawafundisha watu wangu tofauti iliyoko kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida, na kuwafundisha kupambanua kati ya yaliyo machafu na yaliyo safi.


kisha, mpate kupambanua kati ya yaliyo matakatifu na hayo yaliyo ya siku zote, na kati ya yaliyo najisi na hayo yaliyo safi;


ili kufunza itakapokuwa ni unajisi, na itakapokuwa ni safi; hiyo ndiyo sheria ya ukoma.


Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru.


BWANA wa majeshi asema hivi, Ikiwa utaenda katika njia zangu, na kushika maagizo yangu, basi utaihukumu nyumba yangu, na kuzilinda nyua zangu, nami nitakupa haki ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.


Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema.


Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.


kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.


kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.


Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.


Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu.


Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.


Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.


ambao hata saa moja hatukujitia chini yao, ili kwamba kweli ya Injili ikae pamoja nanyi.


Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoeshwa kupambanua mema na mabaya.


Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo