Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yeremia 15:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Mbona maumivu yangu ni ya daima, na jeraha langu halina dawa, linakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe utakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Kwa nini mateso yangu hayaishi? Mbona jeraha langu haliponi, wala halitaki kutibiwa? Ama kweli umenidanganya, kama kijito cha maji ya kukaukakauka!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Kwa nini mateso yangu hayaishi? Mbona jeraha langu haliponi, wala halitaki kutibiwa? Ama kweli umenidanganya, kama kijito cha maji ya kukaukakauka!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Kwa nini mateso yangu hayaishi? Mbona jeraha langu haliponi, wala halitaki kutibiwa? Ama kweli umenidanganya, kama kijito cha maji ya kukaukakauka!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kwa nini maumivu yangu hayakomi, na jeraha langu ni la kuhuzunisha, wala haliponyeki? Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu, kama chemchemi iliyokauka?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kwa nini maumivu yangu hayakomi, na jeraha langu ni la kuhuzunisha, wala haliponyeki? Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu, kama chemchemi iliyokauka?

Tazama sura Nakili

Yeremia 15:18
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika;

Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo; Jeraha langu haliponyeki, nijapokuwa sina makosa.

Na nafsi yangu imefadhaika sana; Na Wewe, BWANA, hadi lini?

Je! Umemkataa Yuda kabisa? Roho yako imeichukia Sayuni? Mbona umetupiga, tusiwe na dawa ya kutuponya? Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yoyote, tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu!

Na wakuu wao huwatuma watoto wao kwenye maji; Nao hufika visimani wasipate maji; Hurudi, na vyombo vyao ni vitupu; Wametahayarika na kufadhaika, Na kuvifunika vichwa vyao.

Nilitoka tumboni kwa sababu gani, kuona taabu na huzuni, hata siku zangu ziharibike katika aibu?

Ee BWANA, umenihadaa, nami nimehadaika; wewe una nguvu kuliko mimi, ukashinda; nimekuwa kitu cha kuchekesha, mchana kutwa; kila mtu hunidhihaki.

Maana BWANA asema hivi, Maumivu yako hayaponyeki, na jeraha lako ni kubwa.

Mbona unalilia maumivu yako? Maumivu yako hayaponyeki; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zimeongezeka, nimekutenda haya.

Kwa hiyo mtaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia; Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.

Kwa maana majeraha yake hayaponyeki; Maana msiba umeijia hata Yuda, Unalifikia lango la watu wangu, Naam, hata Yerusalemu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo