Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 15:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Ndipo BWANA akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Hata kama Mose na Samueli wangesimama mbele yangu na kunisihi, nisingewahurumia watu hawa. Waondoe kabisa mbele yangu. Waache waende zao!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Hata kama Mose na Samueli wangesimama mbele yangu na kunisihi, nisingewahurumia watu hawa. Waondoe kabisa mbele yangu. Waache waende zao!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Hata kama Mose na Samueli wangesimama mbele yangu na kunisihi, nisingewahurumia watu hawa. Waondoe kabisa mbele yangu. Waache waende zao!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia: “Hata kama Musa na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kisha bwana akaniambia: “Hata kama Musa na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende!

Tazama sura Nakili




Yeremia 15:1
32 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za BWANA,


Basi BWANA akakikataa kizazi chote cha Israeli, akawatesa, na kuwatia katika mikono ya watu wenye kuwateka nyara, hata alipokwisha kuwatupa, watoke machoni pake.


Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake na kusimama palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaangamiza.


Musa na Haruni walikuwa makuhani wake, Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake, Walimlilia BWANA naye akawaitikia;


Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali hasira yake itakuwa juu yake aletaye aibu.


Maana BWANA asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu.


Basi, usiwaombee watu hawa, wala usipaze sauti yako, wala kuwaombea dua watu hawa; maana sitawasikia wakati watakaponililia kwa ajili ya taabu yao.


Naye BWANA akaniambia, Usiwaombee watu hawa wapate heri.


Wafungapo, mimi sitasikia kilio chao; na watoapo sadaka za kuteketezwa na sadaka ya unga, sitazitakabali; bali nitawaangamiza kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni.


Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejesha, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.


basi, kwa sababu hiyo, nitawatoeni katika nchi hii, na kuwaingiza katika nchi ambayo hamkuijua, wala ninyi wala baba zenu; na huko mtawatumikia miungu mingine mchana na usiku; kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu hata kidogo.


Maana BWANA asema hivi, Usiingie ndani ya nyumba yenye matanga, wala usiende kuwaombolezea, wala kuwalilia; maana nimewaondolea watu hawa amani yangu, asema BWANA, hata fadhili zangu na rehema zangu.


Je! Mabaya yalipwe badala ya mema? Maana wameichimbia nafsi yangu shimo. Kumbuka jinsi nilivyosimama mbele zako, ili niseme mema kwa ajili yao, nikaigeuze ghadhabu yako isiwapate.


Je! Mtu huyu, Konia, ni chombo kilichodharauliwa, na kuvunjika? Ni chombo kisichopendeza? Mbona wametupwa, yeye na wazao wake, na kutupwa katika nchi wasiyoijua?


basi, kwa hiyo angalieni, nitawasahau ninyi kabisa, nami nitawatupilia mbali, pamoja na mji huu niliowapa ninyi na baba zenu, mtoke mbele za uso wangu;


basi, kwa sababu hiyo, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Yonadabu, mwana wa Rekabu, hatakosa kuwa na mzawa wa kusimama mbele zangu hata milele.


Maana, kwa sababu ya hasira ya BWANA, mambo haya yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata akawaondosha wasiwe mbele za uso wake, naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.


Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu.


wajapokuwa watu hawa watatu, Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu kwa haki yao, asema Bwana MUNGU.


Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.


Uovu wao wote u katika Gilgali; maana huko niliwachukia; kwa sababu ya uovu wa matendo yao nitawafukuza watoke katika nyumba yangu; sitawapenda tena; wakuu wao wote ni waasi.


Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika.


Nikamwomba BWANA, nikasema, Ee Bwana Mungu, usiwaangamize watu wako, urithi wako, uliowakomboa kwa ukuu wako, uliowatoa Misri kwa mkono wa nguvu.


Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;


Moyo wangu unawaelekea makamanda wa Israeli, Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu; Mhimidini BWANA.


Watu wote wakamwambia Samweli, Tuombee watumishi wako kwa BWANA, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.


Lakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka


Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli; BWANA akamwitikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo