Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 13:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Hiyo ndiyo kura yako, fungu lako ulilopimiwa na mimi, asema BWANA; kwa kuwa umenisahau, na kuutumainia uongo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Mwenyezi-Mungu asema: “Hayo ndiyo yatakayokupata, ndivyo nilivyoamua kukutenda mimi Mwenyezi-Mungu, kwa sababu umenisahau mimi, ukaamini miungu ya uongo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Mwenyezi-Mungu asema: “Hayo ndiyo yatakayokupata, ndivyo nilivyoamua kukutenda mimi Mwenyezi-Mungu, kwa sababu umenisahau mimi, ukaamini miungu ya uongo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Mwenyezi-Mungu asema: “Hayo ndiyo yatakayokupata, ndivyo nilivyoamua kukutenda mimi Mwenyezi-Mungu, kwa sababu umenisahau mimi, ukaamini miungu ya uongo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Hii ndiyo kura yako, fungu nililokuamulia,” asema Mwenyezi Mungu, “kwa sababu umenisahau mimi na kuamini miungu ya uongo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Hii ndiyo kura yako, fungu nililokuamuria,” asema bwana, “kwa sababu umenisahau mimi na kuamini miungu ya uongo.

Tazama sura Nakili




Yeremia 13:25
22 Marejeleo ya Msalaba  

Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu, Na urithi aliowekewa na Mungu.


Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.


Wadhalimu wataenda kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.


Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua na kunona kwa mwili wake kutakwisha.


Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;


Naye amewapigia kura, na mkono wake umewagawanyia kwa kamba; wataimiliki hata milele, watakaa ndani yake kizazi hata kizazi.


maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema BWANA, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.


Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.


Maana watu wangu wamenisahau, wameufukizia ubatili uvumba; nao wamewakaza katika njia zao, katika mapito ya zamani, ili wapite katika njia za kando, katika njia isiyotengenezwa;


Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia visima, visima vyenye nyufa visivyoweza kuweka maji.


Je! Mwanamwali aweza kusahau mapambo yake, au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu.


Sauti inasikiwa juu ya vilele vya milima, ni kulia kwao na maombi yao wana wa Israeli; kwa kuwa wameipotosha njia yao, wamemsahau BWANA, Mungu wao.


Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa umenisahau, na kunitupa nyuma yako, basi kwa hiyo, uchukue uasherati wako na uzinzi wako.


Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lolote litakalotufikia.


Hakuitii sauti; hakukubali kurudiwa; hakumwamini BWANA; hakumkaribia Mungu wake.


atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.


Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo