Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 13:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoadoa yake? Kama aweza, ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Je, Mwethiopia aweza kubadili rangi yake, au chui madoadoa yake? Ikiwezekana, nanyi pia mnaweza kutenda mema, nyinyi mliozoea kutenda maovu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Je, Mwethiopia aweza kubadili rangi yake, au chui madoadoa yake? Ikiwezekana, nanyi pia mnaweza kutenda mema, nyinyi mliozoea kutenda maovu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Je, Mwethiopia aweza kubadili rangi yake, au chui madoadoa yake? Ikiwezekana, nanyi pia mnaweza kutenda mema, nyinyi mliozoea kutenda maovu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Je, Mkushi aweza kubadili ngozi yake au chui kubadili madoadoa yake? Vivyo hivyo, wewe uliyezoea kutenda mabaya huwezi kufanya mema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Je, Mkushi aweza kubadili ngozi yake au chui kubadili madoadoa yake? Vivyo hivyo nawe huwezi kufanya mema wewe uliyezoea kutenda mabaya.

Tazama sura Nakili




Yeremia 13:23
13 Marejeleo ya Msalaba  

Walakini hawakusikia, bali wakafanya sawasawa na kawaida zao za kwanza.


Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.


Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki.


Mbona mnataka kupigwa, hata sasa, hata mkazidi kuasi? Kichwa chote ni kigonjwa, moyo wote umezimia.


Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?


Maana ujapojiosha kwa magadi, na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele zangu, asema Bwana MUNGU.


Nimewapiga watoto wako bure; hawakukubali kurudiwa; upanga wenu wenyewe umewala manabii wako, kama simba aharibuye.


Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.


Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.


Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema kweli; wameuzoesha ulimi wao kusema uongo; hujidhoofisha ili kutenda uovu.


Naye Sauli alipoambiwa, alituma wajumbe wengine, wao nao wakatabiri. Naye Sauli akatuma wajumbe tena mara ya tatu, na wao pia wakatabiri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo