Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 13:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Utasema nini wewe, atakapowaweka rafiki zako kuwa kichwa juu yako, ikiwa wewe mwenyewe umewafundisha kuwa juu yako? Je! Huzuni haitakushika, kama uchungu wa mwanamke aliye katika kuzaa?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Utasemaje juu ya wale uliodhani ni rafiki, wale ambao wewe mwenyewe uliwafundisha, watakapokushinda na kukutawala? Je, si utakumbwa na uchungu kama wa mama anayejifungua?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Utasemaje juu ya wale uliodhani ni rafiki, wale ambao wewe mwenyewe uliwafundisha, watakapokushinda na kukutawala? Je, si utakumbwa na uchungu kama wa mama anayejifungua?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Utasemaje juu ya wale uliodhani ni rafiki, wale ambao wewe mwenyewe uliwafundisha, watakapokushinda na kukutawala? Je, si utakumbwa na uchungu kama wa mama anayejifungua?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Utasema nini Mwenyezi Mungu atakapowaweka juu yako wale ulioungana nao kama rafiki zako maalum? Je, hutapatwa na uchungu kama mwanamke aliye katika uchungu wa kuzaa?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Utasema nini bwana atakapowaweka juu yako wale ulioungana nao kama marafiki wako maalum? Je, hutapatwa na utungu kama mwanamke aliye katika utungu wa kuzaa?

Tazama sura Nakili




Yeremia 13:21
17 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Ahazi akatuma wajumbe kwa Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akasema, Mimi ni mtumishi, tena mwana wako; kwea, ukaniokoe mkononi mwa mfalme wa Shamu, na mkononi mwa mfalme wa Israeli, walioniinukia.


Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi?


Nao watafadhaika; watashikwa na uchungu na maumivu; watakuwa na uchungu kama mwanamke aliye karibu kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.


Kwa sababu hiyo viuno vyangu vimejaa maumivu, uchungu umenishika, kama uchungu wa mwanamke azaaye; ninaumwa sana, nisiweze kusikia; nimefadhaishwa wa hofu, nisiweze kuona.


Zuia mguu wako usikose kiatu, na koo yako isiwe na kiu; lakini wewe ulisema, Hakuna matumaini kabisa; la, maana nimewapenda wageni, nami nitawafuata.


Wewe ukaaye Lebanoni, Ujengaye kiota chako katika mierezi, Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana, Upatapo uchungu kama wa mwanamke azaaye.


Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanamume aona uchungu wa uzazi; mbona, basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na uchungu, na nyuso zote zimegeuka rangi?


Tazama, wanawake wote, walioachwa ndani ya nyumba ya mfalme wa Yuda, watatolewa na kuchukuliwa kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, na wanawake hao watasema, Rafiki zako walio karibu wamekudanganya, nao wamekushinda; na kwa kuwa miguu yako imezama matopeni sasa, wamegeuka na kurudi nyuma.


Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako.


Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa uchungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.


Miji imetwaliwa, ngome zimeshambuliwa, na mioyo ya mashujaa wa Moabu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.


Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?


Tumesikia habari zake; mikono yetu inalegea; dhiki imetushika, na uchungu kama wa mwanamke wakati wa kuzaa kwake.


Je! Utazidi kusema mbele yake huyo akuuaye, Mimi ni mungu? Lakini u mwanadamu, wala si Mungu, mkononi mwake akutiaye jeraha.


Hayo yote ndiyo mwanzo wa uchungu.


Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo