Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 12:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Hata lini itaomboleza nchi, na kukauka majani ya nchi yote? Kwa ajili ya mabaya yao wakaao ndani yake, wanyama wameangamia na ndege pia; kwa sababu walisema, Yu kipofu katika njia zetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mpaka lini nchi itaomboleza kwa ukame, na nyasi za mashamba yote kunyauka? Wanyama na ndege wanakufa kwa uovu wa wakazi wake; wanasema: “Mungu hataona mwisho wetu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mpaka lini nchi itaomboleza kwa ukame, na nyasi za mashamba yote kunyauka? Wanyama na ndege wanakufa kwa uovu wa wakazi wake; wanasema: “Mungu hataona mwisho wetu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mpaka lini nchi itaomboleza kwa ukame, na nyasi za mashamba yote kunyauka? Wanyama na ndege wanakufa kwa uovu wa wakazi wake; wanasema: “Mungu hataona mwisho wetu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza hadi lini, na majani katika kila shamba kunyauka? Kwa sababu wale wanaoishi ndani yake ni waovu, wanyama na ndege wameangamia. Zaidi ya hayo, watu wanasema, “Mwenyezi Mungu hataona yatakayotupata sisi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini, na majani katika kila shamba kunyauka? Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu, wanyama na ndege wameangamia. Zaidi ya hayo, watu wanasema, “bwana hataona yatakayotupata sisi.”

Tazama sura Nakili




Yeremia 12:4
22 Marejeleo ya Msalaba  

Nchi ya matunda mengi ikawa uwanda wa chumvi, Kwa sababu ya uovu wa wakazi wake.


Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe. Lakini nitakukemea; Nitakuhukumu kwa hayo yote.


Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika.


Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.


Wamelifanya kuwa ukiwa, na kwa kuwa ni ukiwa linanililia; nchi yote imefanywa kuwa ukiwa, kwa sababu hapana mtu aliyeweka haya moyoni mwake.


Yuda huomboleza, Na malango yake yamelegea; Wameketi chini wamevaa kaniki; Na kilio cha Yerusalemu kimepaa juu.


Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki.


Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao.


Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi; kwa sababu mimi nimeyanena haya, na kuyakusudia, wala sikujuta wala mimi sitarudi nyuma niyaache.


na manabii watakuwa upepo, wala neno lake halimo ndani yao; basi ndivyo watakavyotendwa.


Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?


Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.


Kwa milima nitalia na kulalama, Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo; Kwa sababu yameteketea, hata hakuna apitaye, Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng'ombe; Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, Wamekimbia, wamekwenda zao.


Je! Nisiwaadhibu kwa mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?


Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa porini na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataangamizwa.


Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng'ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamehangaika.


Naye alisema, BWANA atanguruma toka Sayuni, Atatoa sauti yake toka Yerusalemu; Na malisho ya wachungaji yatakauka, Na kilele cha Karmeli kitanyauka.


Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe;


Ndipo yule malaika wa BWANA akajibu, akasema, Ee BWANA wa majeshi, hadi lini utakataa kuurehemu Yerusalemu, na miji ya Yuda uliyoikasirikia miaka hii sabini?


Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina uchungu pamoja hata sasa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo