Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 12:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Wamepanda ngano, lakini watavuna miiba; wamejiumiza nafsi zao, lakini hawatakuwa na faida; naam, tahayarini kwa ajili ya matunda yenu, kwa sababu ya hasira kali ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Walipanda ngano, lakini walivuna magugu; walifanya bidii, lakini hawakupata kitu. Kwa sababu ya hasira yangu kali, mavuno watakayoyapata yatakuwa aibu tupu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Walipanda ngano, lakini walivuna magugu; walifanya bidii, lakini hawakupata kitu. Kwa sababu ya hasira yangu kali, mavuno watakayoyapata yatakuwa aibu tupu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Walipanda ngano, lakini walivuna magugu; walifanya bidii, lakini hawakupata kitu. Kwa sababu ya hasira yangu kali, mavuno watakayoyapata yatakuwa aibu tupu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Watapanda ngano lakini watavuna miiba; watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote. Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako kwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Watapanda ngano lakini watavuna miiba; watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote. Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako kwa sababu ya hasira kali ya bwana Mwenyezi Mungu.”

Tazama sura Nakili




Yeremia 12:13
19 Marejeleo ya Msalaba  

Akawatoa watu wake wapigwe kwa upanga; Akaughadhibikia urithi wake.


Kwa nini mtoe fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.


Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.


Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za BWANA, na mbele za hasira yake kali.


Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema kweli; wameuzoesha ulimi wao kusema uongo; hujidhoofisha ili kutenda uovu.


Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.


mimi nami nitawatenda jambo hili; nitaamrisha uje juu yenu utisho, hata kifua kikuu na homa, zitakazoharibu macho yenu, na kuidhoofisha roho; nanyi mtapanda mbegu yenu bure, kwa kuwa adui zenu wataila.


na nguvu zenu mtazitumia bure; kwa kuwa nchi yenu haitazaa mazao yake, wala miti ya nchi haitazaa matunda yake.


Utapanda, lakini hutavuna; utazikanyaga zeituni, lakini hutajipaka mafuta; na hizo zabibu, lakini hutakunywa divai.


Angalieni; je! Jambo hili halikutoka kwa BWANA wa majeshi, kwamba watu wajishughulikie moto, na mataifa wajisumbue kwa ajili ya ubatili?


Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamtosheki na vinywaji; mnajivika nguo lakini hampati joto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotobokatoboka.


Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha mbali. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu yumba yangu imebaki kuwa gofu la nyumba, wakati ambapo kila mmoja wenu anakimbilia nyumbani kwake.


Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.


Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo