Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 10:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa BWANA; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Nami Yeremia nikasema: Wachungaji wamekuwa wajinga, hawakuomba shauri kwa Mwenyezi-Mungu; kwa sababu hiyo, hawakufanikiwa, na kondoo wao wote wametawanyika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Nami Yeremia nikasema: Wachungaji wamekuwa wajinga, hawakuomba shauri kwa Mwenyezi-Mungu; kwa sababu hiyo, hawakufanikiwa, na kondoo wao wote wametawanyika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Nami Yeremia nikasema: Wachungaji wamekuwa wajinga, hawakuomba shauri kwa Mwenyezi-Mungu; kwa sababu hiyo, hawakufanikiwa, na kondoo wao wote wametawanyika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Wachungaji hawana akili wala hawamuulizi Mwenyezi Mungu, hivyo hawastawi na kundi lao lote la kondoo limetawanyika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Wachungaji hawana akili wala hawamuulizi bwana, hivyo hawastawi na kundi lao lote la kondoo limetawanyika.

Tazama sura Nakili




Yeremia 10:21
18 Marejeleo ya Msalaba  

Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.


Lakini wote pia huwa kama wanyama, ni wapumbavu. Haya ni maelezo ya sanamu, ni shina la mti tu.


Wachungaji wengi wameliharibu shamba langu la mizabibu, wamelikanyaga fungu langu chini ya miguu yao, wamefanya fungu langu zuri kuwa jangwa la ukiwa.


Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wanasheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.


BWANA asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.


Na ngamia wao watakuwa mateka, na wingi wa makundi yao utakuwa nyara; nami nitawatawanya katika pande zote watu wale wanyoao denge; nami nitaleta msiba wao toka pande zao zote, asema BWANA.


Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?


Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadneza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.


Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la BWANA, wana akili gani ndani yao?


Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo wake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo wake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu; nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza.


Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji, nami nitawaadhibu viongozi; kwa maana BWANA wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani.


Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema BWANA wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo