Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 10:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Maana BWANA asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii, nitawataabisha asibaki mtu yeyote.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii, nitawataabisha asibaki mtu yeyote.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii, nitawataabisha asibaki mtu yeyote.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu wote wanaoishi katika nchi hii; nitawataabisha ili wapate kutekwa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kwa kuwa hili ndilo asemalo bwana: “Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu wote waishio katika nchi hii; nitawataabisha ili waweze kutekwa.”

Tazama sura Nakili




Yeremia 10:18
11 Marejeleo ya Msalaba  

Tazama, BWANA atakutupa kwa nguvu, kama mtu mwenye nguvu; naam, atakuzongazonga.


basi, kwa sababu hiyo, nitawatoeni katika nchi hii, na kuwaingiza katika nchi ambayo hamkuijua, wala ninyi wala baba zenu; na huko mtawatumikia miungu mingine mchana na usiku; kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu hata kidogo.


Nami nitakutupa nje, wewe na mama yako aliyekuzaa, mwende katika nchi nyingine ambayo hamkuzaliwa huko, nanyi mtakufa huko.


Hasira ya BWANA haitarudi, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtalifahamu neno hili kabisa.


Nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA; sikusema bure kama nitawatenda mabaya hayo.


Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.


Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.


Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa BWANA, Mungu wako.


Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na BWANA, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya kombeo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo