Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 10:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Binadamu ni mjinga na mpumbavu; kila mfua dhahabu huaibishwa na vinyago vyake; maana, vinyago hivyo ni uongo mtupu. Havina uhai wowote ndani yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Binadamu ni mjinga na mpumbavu; kila mfua dhahabu huaibishwa na vinyago vyake; maana, vinyago hivyo ni uongo mtupu. Havina uhai wowote ndani yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Binadamu ni mjinga na mpumbavu; kila mfua dhahabu huaibishwa na vinyago vyake; maana, vinyago hivyo ni uongo mtupu. Havina uhai wowote ndani yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kila mtu ni mjinga na hana maarifa; kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. Vinyago vyake ni vya udanganyifu; havina pumzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kila mmoja ni mjinga na hana maarifa, kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. Vinyago vyake ni vya udanganyifu, havina pumzi ndani yavyo.

Tazama sura Nakili




Yeremia 10:14
20 Marejeleo ya Msalaba  

Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu.


Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu.


Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini; Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?


Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.


Hakika nimekuwa kama mnyama, wala si mtu; Wala sina ufahamu wa mwanadamu;


Watarudishwa nyuma, wataaibishwa sana, hao wanaotumainia sanamu za mawe, na kuziambia sanamu za madini, Ninyi ndinyi miungu yetu.


Tazama, wenziwe wote watatahayari; na mafundi, hao ni wanadamu; na wakusanyike pamoja, wakasimame; wataogopa na kutahayari pamoja.


Watatahayarika, naam, watafadhaika, wote pia; wale watengenezao sanamu wataingia fadhaa pamoja.


Mimi nitatangaza haki yako, na matendo yako hayatakufaa.


Mfano wao ni mfano wa mtende, kazi ya cherehani, hawasemi; hawana budi kuchukuliwa, kwa sababu hawawezi kwenda. Usiwaogope; kwa maana hawawezi kutenda uovu, wala hawana uwezo wa kutenda mema.


Lakini wote pia huwa kama wanyama, ni wapumbavu. Haya ni maelezo ya sanamu, ni shina la mti tu.


Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.


Hata walipoamka kesho yake asubuhi, kumbe! Dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA; na kichwa chake Dagoni na vitanga vyote viwili vya mikono yake vimekatika, na kulazwa kizingitini; Dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo