Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wimbo Ulio Bora 7:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Twende mapema hadi mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabibu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa upendo wangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu, tukaone kama imeanza kuchipua, na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua, pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua. Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu, tukaone kama imeanza kuchipua, na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua, pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua. Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu, tukaone kama imeanza kuchipua, na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua, pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua. Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Hebu na twende mapema katika mashamba ya mizabibu tuone kama mizabibu imechipua, kama maua yake yamefunguka, na kama mikomamanga imetoa maua: huko nitakupa penzi langu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Hebu na twende mapema katika mashamba ya mizabibu tuone kama mizabibu imechipua, kama maua yake yamefunguka, na kama mikomamanga imetoa maua: huko nitakupa penzi langu.

Tazama sura Nakili




Wimbo Ulio Bora 7:12
27 Marejeleo ya Msalaba  

Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya ukoo wa Daudi.


Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.


Ni nani niliye naye mbinguni, Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.


Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.


Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.


Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.


Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.


Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua.


Machipuko yako ni bustani ya komamanga, Yenye matunda mazuri, hina na nardo,


Amka, kaskazi; nawe uje, kusi; Vumeni juu ya bustani yangu, Manukato ya bustani yatokee. Mpendwa wangu na aingie bustanini mwake, Akayale matunda yake mazuri.


Nilishukia katika bustani ya milozi, Ili kuyatazama machipuko ya bondeni; Nione kama mzabibu umechanua, Kama mikomamanga imetoa maua.


Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji.


Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu, Mapenzi katikati ya anasa!


Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata.


Baada ya siku kadhaa Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Turejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wako hali gani.


Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.


Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa.


Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo kwa upendo usioisha.


mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.


Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.


awaache huru wale ambao katika maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.


Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo