Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wimbo Ulio Bora 5:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Mikono yake ni kama mianzi ya dhahabu, lliyopambwa kwa zabarajadi; Kiwiliwili chake kama kazi ya pembe, Iliyonakishiwa kwa yakuti samawi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mikono yake imewekwa bangili za dhahabu, amevalia johari za Tarshishi. Kiwiliwili chake ni kama pembe za ndovu zilizopambwa kwa vito vya johari ya rangi ya samawati.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mikono yake imewekwa bangili za dhahabu, amevalia johari za Tarshishi. Kiwiliwili chake ni kama pembe za ndovu zilizopambwa kwa vito vya johari ya rangi ya samawati.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mikono yake imewekwa bangili za dhahabu, amevalia johari za Tarshishi. Kiwiliwili chake ni kama pembe za ndovu zilizopambwa kwa vito vya johari ya rangi ya samawati.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Mikono yake ni fimbo za dhahabu iliyopambwa kwa krisolitho. Mwili wake ni kama pembe ya ndovu iliyong’arishwa iliyopambwa na yakuti samawi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Mikono yake ni fimbo za dhahabu iliyopambwa kwa krisolitho. Mwili wake ni kama pembe ya ndovu iliyong’arishwa iliyopambwa na yakuti samawi.

Tazama sura Nakili




Wimbo Ulio Bora 5:14
15 Marejeleo ya Msalaba  

Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti samawi.


Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki; Umeiimarisha haki; Umefanya hukumu na haki katika Israeli.


BWANA, mkono wako wa kulia umepata fahari ya uwezo, BWANA, mkono wako wa kulia wawasetaseta adui.


wakamwona Mungu wa Israeli; chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi, kama zile mbingu zenyewe kwa usafi wake.


na safu ya pili itakuwa zumaridi, na yakuti samawi, na almasi;


na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, shohamu na yaspi; vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake.


Na safu ya nne ilikuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi: vito hivyo vilikuwa vimetiwa katika vijalizo vya dhahabu, kila kimoja mahali pake.


Kitovu chako ni kama bakuli la mviringo, Na isikose divai iliyochanganyika; Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano, Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro;


Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.


Ewe uliyeteswa, uliyerushwa na tufani, usiyetulizwa, tazama, nitaweka mawe yako kwa rangi nzuri, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.


Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima, Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.


Kuonekana kwake magurudumu hayo na kazi yake kulikuwa kama rangi ya zabarajadi; nayo yote manne yalikuwa na mfano mmoja; na kuonekana kwake na kazi yake kulikuwa kana kwamba ni gurudumu ndani ya gurudumu lingine.


mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo