Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wimbo Ulio Bora 4:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Bibi arusi, njoo pamoja nami toka Lebanoni, Pamoja nami toka Lebanoni. Shuka kutoka kilele cha Amana, Kutoka vilele vya Seniri na Hermoni; Kutoka mapangoni mwa simba, Kutoka milimani mwa chui.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Njoo, bibiarusi wangu tuondoke Lebanoni; na tuiachilie mbali Lebanoni. Shuka toka kilele cha mlima Amana, toka kilele cha Seniri na Hermoni, toka mapango ya simba, toka milima ya chui.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Njoo, bibiarusi wangu tuondoke Lebanoni; na tuiachilie mbali Lebanoni. Shuka toka kilele cha mlima Amana, toka kilele cha Seniri na Hermoni, toka mapango ya simba, toka milima ya chui.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Njoo, bibiarusi wangu tuondoke Lebanoni; na tuiachilie mbali Lebanoni. Shuka toka kilele cha mlima Amana, toka kilele cha Seniri na Hermoni, toka mapango ya simba, toka milima ya chui.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Nenda nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu, nenda nami kutoka Lebanoni. Shuka kutoka ncha ya Amana, kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni, kutoka mapango ya simba na kutoka mlima wapendapo kukaa chui.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Enda nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu, enda nami kutoka Lebanoni. Shuka kutoka ncha ya Amana, kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni, kutoka mapango ya simba na kutoka mlima wapendapo kukaa chui.

Tazama sura Nakili




Wimbo Ulio Bora 4:8
19 Marejeleo ya Msalaba  

Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.


Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira.


Na wana wa nusu kabila la Manase walikaa katika nchi; nao wakaongezeka kutoka Bashani mpaka Baal-hermoni, na Seniri, na mlima Hermoni.


Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako.


Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawayewaye kama ilivyo katika milima ya Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi.


Katika Yuda Mungu amejulikana, Katika Israeli jina lake ni kuu.


Wewe U mwenye fahari na adhama, Toka milima ya mateka.


Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba, Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.


Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu.


Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.


Naingia bustanini mwangu, dada yangu, bibi arusi, Nachuma manemane yangu na rihani, Nala sega la asali na asali yangu, Nanywa divai yangu na maziwa. Kaleni, rafiki zangu, kanyweni, Naam, nyweni sana, wapendwa wangu.


Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji.


Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.


Mbao zako zote wamezifanya kwa misonobari itokayo Seniri; wametwaa mierezi ya Lebanoni ili kukufanyia mlingoti;


Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Nami nakuomba nivuke, nikaione hiyo nchi nzuri iliyoko ng'ambo ya Yordani, mlima ule mzuri, na Lebanoni.


(na hiyo Hermoni Wasidoni huiita Sirioni, na Waamori huiita Seniri);


Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng'ambo ya pili ya Yordani, upande wa maawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo