Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wimbo Ulio Bora 4:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua, Nyuma ya barakoa yako. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, Wakijilaza mbavuni pa mlima Gileadi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Hakika u mzuri ewe mpenzi wangu, hakika u mzuri! Macho yako ni kama ya hua nyuma ya shela lako, nywele zako ni kama kundi la mbuzi washukao katika milima ya Gileadi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Hakika u mzuri ewe mpenzi wangu, hakika u mzuri! Macho yako ni kama ya hua nyuma ya shela lako, nywele zako ni kama kundi la mbuzi washukao katika milima ya Gileadi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Hakika u mzuri ewe mpenzi wangu, hakika u mzuri! Macho yako ni kama ya hua nyuma ya shela lako, nywele zako ni kama kundi la mbuzi washukao katika milima ya Gileadi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpendwa wangu! Ee, jinsi ulivyo mzuri! Macho yako nyuma ya shela yako ni kama ya hua. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi wakishuka kutoka Mlima Gileadi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Ee, jinsi ulivyo mzuri! Macho yako nyuma ya shela yako ni kama ya hua. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi zikishuka kutoka Mlima Gileadi.

Tazama sura Nakili




Wimbo Ulio Bora 4:1
17 Marejeleo ya Msalaba  

Naye mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie.


Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua.


Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako,


Hua wangu, mafichoni mwa jabali, Katika sitara za, magenge Nitazame uso wako, nisikie sauti yako, Maana sauti yako ni tamu na uso wako unapendeza.


Uyageuzie macho yako mbali nami, Kwa maana yamenitisha sana. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, Wakijilaza mbavuni pa Gileadi.


Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga, Nyuma ya barakoa yako.


Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli, Na nywele za kichwa chako kama urujuani, Mfalme amenaswa na mashungi yake.


Kwa maana BWANA asema hivi, kuhusu habari za nyumba ya mfalme wa Yuda; Wewe u Gileadi kwangu, na kichwa cha Lebanoni; Ila hakika nitakufanya kuwa jangwa, na miji isiyokaliwa na watu.


Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana MUNGU.


Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, msituni katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale.


Basi wana wa Reubeni, na hao wana wa Gadi, walikuwa na wanyama wa mifugo wengi sana; nao walipoona nchi ya Yazeri, na nchi ya Gileadi, ya kuwa mahali hapo palikuwa ni mahali pa kuwafaa wanyama;


Basi Musa akampa Makiri, mwana wa Manase, Gileadi, naye akakaa humo.


Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;


Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo