Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wimbo Ulio Bora 3:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Usiku kitandani nilimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nilimtafuta, nisimpate.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Usiku nikiwa kitandani mwangu, niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu; nilimtafuta, lakini sikumpata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Usiku nikiwa kitandani mwangu, niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu; nilimtafuta, lakini sikumpata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Usiku nikiwa kitandani mwangu, niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu; nilimtafuta, lakini sikumpata.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Usiku kucha kwenye kitanda changu nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Usiku kucha kwenye kitanda changu nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata.

Tazama sura Nakili




Wimbo Ulio Bora 3:1
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha.


Muwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.


Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakibubujikia kitanda changu; Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.


Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa shela, Karibu na makundi ya wenzako?


Nilimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita; (Nimezimia nafsi yangu aliponena), Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie.


Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Ninyi mkimwona mpendwa wangu, Ni nini mtakayomwambia? Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.


Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.


Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yuko karibu;


Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.


Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea.


Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.


Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo