Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wimbo Ulio Bora 2:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake; Hulisha kundi lake penye nyinyoro.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake. Yeye hulisha kondoo wake penye yungiyungi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake. Yeye hulisha kondoo wake penye yungiyungi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake. Yeye hulisha kondoo wake penye yungiyungi,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake, yeye hujilisha kati ya yungiyungi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake, yeye hujilisha katikati ya yungiyungi.

Tazama sura Nakili




Wimbo Ulio Bora 2:16
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.


Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.


Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa shela, Karibu na makundi ya wenzako?


Mimi ni ua la uwandani, Ni fahirisi ya mabondeni.


Matiti yako mawili ni kama wanapaa wawili, Nyuma ya barakoa yako. Ambao ni mapacha ya paa; Wakilisha penye nyinyoro.


Mpendwa wangu ameshukia bustani yake, Kwenye matuta ya rihani; Ili kulisha penye bustani, Ili kuchuma nyinyoro.


Mimi ni wake mpendwa wangu, naye ni wangu, Hulisha kundi lake penye nyinyoro.


Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu.


Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji.


Mitunguja hutoa harufu yake; Juu ya milango yetu yako matunda mazuri, Mapya na ya kale, ya kila namna, Niliyokuwekea, mpendwa wangu.


Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.


Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.


Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo