Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wimbo Ulio Bora 1:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutalinena pendo lako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Nichukue, twende zetu haraka, mfalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wanawake wana haki kukupenda!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Nichukue, twende zetu haraka, mfalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wanawake wana haki kukupenda!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Nichukue, twende zetu haraka, mfalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wanawake wana haki kukupenda!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako kuliko divai. Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!

Tazama sura Nakili




Wimbo Ulio Bora 1:4
37 Marejeleo ya Msalaba  

Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; BWANA ni mwenye fadhili na rehema.


Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako, Utakaponipanulia ufahamu wangu.


Nilifanya haraka wala sikukawia, Kuyatii maagizo yako.


Israeli na amfurahie Yeye aliyemwumba, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.


Nayakumbuka mambo haya kwa uchungu moyoni mwangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza hadi katika nyumba ya Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.


Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, Katikati ya hekalu lako.


Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.


Kitambo kidogo tu nilipoachana nao, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa.


Jinsi pendo lako lilivyo nzuri, dada yangu, Bibi arusi, ni nzuri kupita divai; Na harufu ya marhamu yako Yapita manukato ya kila namna.


Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.


Katika BWANA wazao wote wa Israeli watapewa haki, na kutukuka.


kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.


Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.


BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.


Niliwavuta kwa kamba za kibinadamu, kwa mafungo ya upendo; nami nilikuwa kwao kama hao waondoao kongwa tayani mwao, nikaandaa chakula mbele yao.


Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli; Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti Yerusalemu.


Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.


Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.


Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;


Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.


Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.


Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenituma; nami nitamfufua siku ya mwisho.


Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;


Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo kwa upendo usioisha.


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.


Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.


Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa subira katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,


Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo