Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waroma 8:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukingojea tufanywe watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukingojea tufanywe watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukingojea tufanywe watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Wala si hivyo viumbe peke yao, bali hata sisi ambao ndio matunda ya kwanza ya Roho wa Mungu, kwa ndani tunalia kwa uchungu tukisubiri kwa shauku kufanywa wana wa Mungu, yaani ukombozi wa miili yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Wala si hivyo viumbe peke yao, bali hata sisi ambao ndio matunda ya kwanza ya Roho, kwa ndani tunalia kwa uchungu tukisubiri kwa shauku kufanywa wana wa Mungu, yaani, ukombozi wa miili yetu.

Tazama sura Nakili




Waroma 8:23
26 Marejeleo ya Msalaba  

Mara amri ilipovavagaa, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, divai, mafuta, asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta kwa wingi.


wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.


Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.


Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.


Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta subira;


na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.


Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?


Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.


hata hamkupungukiwa na karama yoyote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;


naye ndiye aliyetutia mhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.


Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tuliteseka kotekote; nje palikuwa na vita, ndani hofu.


Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.


Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.


Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa mhuri hata siku ya ukombozi.


kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;


baada ya hayo nimewekewa taji la haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.


tukilitazamia tumaini lenye baraka na kufunuliwa kwa utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;


kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.


ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.


Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini tunajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo